Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mratibu wa Kimataifa wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani katika mwitikio wa kupambana na Ukimwi (PEPFAR) na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya Marekani katika masuala ya Diplomasia ya Afya Balozi Dkt. John Nkengasong,  pamoja na Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) Bw. Peter Sands,  Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 12 Juni 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na Mratibu wa Kimataifa wa Mpango wa Dharura wa Rais wa Marekani katika mwitikio wa kupambana na Ukimwi (PEPFAR) na Mwakilishi Maalum wa Serikali ya Marekani katika masuala ya Diplomasia ya Afya Balozi Dkt. John Nkengasong, Mwakilishi Maalum wa Global Health Diplomacy na Mshauri wa masuala ya Mawasiliano US AIDS Bibi Veronica Davison, Mtendaji Mkuu wa Shirika la Kimataifa la kupambana na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria (Global Fund) Bw. Peter Sands, Katibu Mkuu Kiongozi Dkt. Moses Kusiluka na Waziri wa Afya Mhe. Ummy Mwalimu, mara baada ya mazungumzo yao  Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma tarehe 12 Juni 2023.