Na Mwandishi Wetu

Uongozi wa Young Africans Sports Club umesema kuwa umemuuza Mchezaji Feisal Salum “Fei Toto” kwa Kilabu ya Azam FC kwa dau ambalo halitawekwa wazi.

Kwa Mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma Leo Juni 8, 2023, kilabu hiyo imeeleza kuwa, hatua hiyo ni baada ya mazungumzo ya pande zote mbili kukamilika kwa kuzingatia matakwa ya klabu na mchezaji.

Aidha Klabu hiyo imesema kuwa Fei Toto ataungana na timu yake mpya ya Azam Fc baada ya makubaliano binafsi na dirisha la usajili kufunguliwa.

Itakumbukwa Mnamo June 5, 2023 Rais wa jamhuri ya Tanzania Saimia Suluhu Hassan aliiomba Kilabu ya Yanga kumaliza mgogoro kati ya kilabu na mchezaji huyo, ambapo kwa muda murefu mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja kwa kile kilichodaiwa kuwa na mgogoro na Yanga hata hivyo yeye mwenyewe alieleza wazi kutofautiana na Rais wa kilabu hiyo Mhandisi Hersi Said.

By Jamhuri