Waziri wa Nishati January Makamba amesema wanaridhishwa na kasi ya Ujazaji maji Bwawa la kuzalisha Umeme la Mwalimu Nyerere Hydro Power.

Kwa sasa ujazo wa maji umefika lita Bilioni Sita huku kukiwa kumebaki mita kumi na tatu tu, kufikia Kiwango cha Maji yatakayoweza kuzungusha mitambo ya kufua Umeme.

Waziri Makamba amesema kuwa kiwango hiko ni kizuri na kimezidi matarajio yaliyokuwepo awali wakati wa uzinduzi wa ujazaji maji uliofanywa na Rais Samia Suluhu Hassan na kusema “Maendeleo mazuri ingawa kazi bado ipo.

Kwa mujibu wa takwimu,wiki mbili zilizopita kiwango maji yameingia mengi kuliko yaliyoleta mafuriko 2019/2020. Hii maana yake neema iliyopo kwa sasa zile athari za mafuriko hazipo tena.

“Bwawa hili limeanza kuzaa matunda tuliyotarajia ikiwemo kudhibiti mafuriko. Kwa sasa tuko asimilia 86 wakati Rais Samia anachukua madaraka ya nchi mradi huu ulikua ni asilimia 37” alisema Waziri Makamba.

By Jamhuri