Makamu mwenyekiti CCM Z’Bar audhuria mkutano wa 10 Dodoma

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akifurahia jambo na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Philip Isdor Mpango, wakiwa katika ukumbi wa mkutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, wakati wa Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM uliofanyika leo 8-12-2022. (Picha na Ikulu)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Mstaafu Mhe.Dk.Ali Mohamed Shein, alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma,wakati wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama cha Mapinduzi, uliofanyika leo 8-12-2022.(Picha na Ikulu)
Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza Rais Mstaafu wa Tanzania Mhe.Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete, wakiwa katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, kabla ya kuaza kwa Mkutano Mkuu wa 10 wa CCM uliofanyika leo 8-12-2022 katika ukumbi huo na (kulia kwa Rais) Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ambae pia ni Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe.Philip Isdor Mpango.(Picha na Ikulu)
Makamu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar ambae pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, alipowasili katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete Jijini Dodoma, kuongoza Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi uliofanyika katika ukumbi huo leo 8-12-2022.(Picha na Ikulu)
Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa 10 wa Chama Cha Mapinduzi wakiwa katika ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Mrisho Kikwete, wakati Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambae pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Wajumbe wa Mkutano huo uliyofanyika leo 8-12-2022.(Picha na Ikulu)