Na Aziza Nangwa, JamhuriMedia, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi, ameiagiza Wizara ya Nishati kupitia Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) kuandaa mpango mkakati wa kuwajengea uwezo vijana na kampuni za Kitanzania ili washiriki kikamilifu katika miradi ya mafuta na gesi asilia.

Ndejembi ametoa maelekezo hayo leo, Oktoba 28, 2026, jijini Dar es Salaam, katika hafla ya utiaji saini leseni za utafutaji wa mafuta na gesi.

Amesema kwa sasa lazima kuwepo maandalizi ya vijana hao ili , kabla miradi mikubwa ikiwemo mradi wa LNG mkoani Lindi wakati haijakamilika, ili Watanzania wawe tayari kushiriki kama wataalamu, watoa huduma na
wasambazaji wa bidhaa

Makamu wa Rais alitolea mfano kijana wa kitanzania Mwizegwa Rusibamanyila, aliyeacha kazi nje ya nchi na kurudi nyumbani kuanzisha kampuni inayofanya kazi katika kitalu cha gesi cha Mnazi Bay, mkoani Mtwara.

Ndejembi amesema kwa sasa Kampuni hiyo imeajiri zaidi ya Watanzania 50, na asilimia 80 kati yao wanatoka katika kijiji kinachozunguka mradi huo.

Miongoni mwao ni binti aliyeajiriwa akiwa bado mwanafunzi, akaendelezwa kielimu, na sasa ni mmoja wa wasimamizi wa mradi huo.

“Kitengo cha local content tukikisimamia vizuri, tuna uwezo wa kuzalisha akina Rusibamanyila wengi zaidi ambao watakuja kuajiri Watanzania wenzao katika miradi ya mafuta na gesi,” amesema

Aidha, amemshauri Waziri wa Nishati kuandaa tuzo maalum kwa kijana huyo kutokana na kazi kubwa anayoifanya.