Makinda: Sensa ya 2032 inategemea kujikosoa kwa sensa ya 2022

Kamisaa wa Sensa Anne Makinda ameeleza ,Maandalizi ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2032 inategemea mafanikio na ufumbuzi wa changamoto zilizojitokeza sensa ya mwaka 2022 ili kuleta matokeo chanya.

Ameelezea kwamba,ameshukuru Sensa hii imefanywa kwa uzalendo na wananchi walikuwa na muitiko mkubwa.

Akizungumza na Kamati ya Sensa mkoa wakati akipokea taarifa ya sensa mkoa wa Pwani, Makinda alisema ni mkoa wa kwanza baada ya Zoezi hilo kukamilika, kuelekea kwenye taarifa sahihi na ya kina ya sensa itakayotolewa na mh.Rais Samia Suluhu Hassan mwezi octoba mwaka huu.

Alieleza maandalizi na matokeo mazuri ya sensa ya mwaka 2032 yanatokana na kujifunza kutokana na changamoto zilizojitokeza sasa ili kujikosoa.

Hata hivyo Makinda alisema ,Zoezi limefanikiwa kwa asilimia 99.99 na mikoa Kama mkoa wa Pwani wenye asilimia 136 ambayo asilimia zimezidi imetokana na makisio Yao waliyojiwekea kabla ya zoezi kukamilika.
Vilevile alisema kwamba, Takwimu zilizopo zisaidie kuanzia ngazi ya chini kwa kutumia data ili kupanga mipango ya maendeleo na Serikali kujifunza kupanga miji yake.

“Kwetu sisi hatuna tamaduni ya kutumia takwimu, tujifunze na sisi kujiendeleza,kupanga mipango kwa kutumia data.

“Kuwa na idadi kamili ya wamachinga, wafanyabiashara, kundi la walemavu,watoto wa kike wanaoelekea kuzaa kujua idadi Yao,magorofa mangapi ,nyumba za kawaida ngapi ili kupanga mpango mzuri wa Maendeleo mbalimbali, miundombinu ya maji,umeme,maji taka na mengine “alibainisha Makinda.

“Tunashukuru mfumo ulikuwa mzuri, wakuu wa mikoa walishiriki kikamilifu kutatua changamoto zilizopo ikiwemo usafiri,na wananchi walijitoa Sana , wengine walipiga simu kuwa Mimi sijahesabiwa ,”!Ni sensa iliyofanyika kwa uzalendo:.alifafanua Makinda.

Makinda alielezea ,Vishkwambi vinarudishwa katika Taasisi husika ikiwemo UNICEF,NBS,Wizara ya elimu na Kama vimeharibika vitengenezwe ,kwani Kama vya NBS vinarudishwa kuendelea na tafiti nyingine.

Wakati huo huo, aliwaasa wananchi waache kulalamika kuwa Hali ngumu badala yake wajitume ,wasichague kazi ili kujiongezea kipato.
Awali Mkuu wa mkoa wa Pwani, alhaj Abubakari Kunenge alisema Zoezi la sensa Mkoani humo limefanikiwa kwa asilimia 136.

Alieleza,wilaya ya Mkuranga imeonekana Kuwa idadi kubwa ya watu hali iliyosababisha kuongeza nguvu ya makarani kutoka wilaya nyingine ili kufanikisha zoezi hilo.

Kunenge alieleza, mkoa huo walikuwa wakichangia pato la taifa 1.94 kwa mwaka 2018 hivyo wanaamini baada ya kupata picha halisi ya takwimu ya watu na makazi pato litapanda.

Mratibu wa sensa mkoa wa Pwani,Adella Temba ,alitaja changamoto kwa baadhi ya maeneo kuwa na idadi kubwa ya kaya na majengo ya kuhesabu isiyoendana na idadi ya makarani waliopangwa hasa katika Halmashauri ya Mkuranga.

Alieleza, wakufunzi 81 kutoka Kisarawe, Bagamoyo, Kibiti, Kibaha Mji na Dar es Salaam ,”makarani 50 kutoka Kisarawe na 600 kutoka Dar es Salaam maeneo ya Temeke,Twangoma, Mbagala, Chang’ombe,Manzese na Kijitonyama walihamishiwa Mkuranga kwa ajili ya kuongeza nguvu kazi.

Adella alipendekeza, wataalamu wa GIS wafanye mapitio ya maeneo yaliyotengwa (EA) ili kutoleta changamoto kwenye tafiti zijazo.

Changamoto nyingine ni baadhi ya wananchi kutopatikana majumbani ,vishkwambi kutokuwa na uwezo wa kutunza chaji kwa muda mrefu kiasi cha kuathiri Zoezi siku ya kwanza, baadhi ya kaya kutojua lugha ya Taifa na kusababisha makarani kutumia wakalimani, Changamoto ya mipaka na maeneo mengine kuwa makubwa kijografia huku baadhi ya maeneo hayakuwekwa kwenye ramani za kuhesabiwa watu.