Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar

Chama cha Mapinduzi (CCM), Taifa kimesema kuwa tatizo la kukatika kwa umeme limekuwa ni changamoto kubwa kwa wananchi na hivyo kimewataka watendaji wa Shirika la umeme nchini TANESCO kujitathimini.

Kimesema kuwa hakuna haja ya kutafuna ama kumung’unya maneno kwani ifike mahala lazima kusema ukweli tatizo la umeme limekuwa ni sugu sio tu Kwa wananchi wakawaida.lakini hata Kwa viongozi kwani na wenyewe wanaishi mtaani kama ilivyo wananchi wakawaida.

Kauli hiyo imetolewa Jijini Dar es Salaam leo Desemba 21, 2023 na na Katibu wa Itikadi ,Uenezi na Mafunzo wa Chama hicho Paul Makonda katika mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ofisi ndogo za chama hicho Lumumba jijini Dar es Salaam.

“Chama cha Mapinduzi kinaona changamoto hiyo ya umeme na hapo lazima waseme ukweli hasa Kwa watendaji wa Shirika la umeme nchini TANESCO kujitathimini kwani haiwezikani Mwenyekiti hadi analazimika kuvunja hadi Bodi kwasababu uwajibikaji mdogo wa watendaji hivyo hata watendaji wa TANESCO kama wameshindwa basi wanatakiwa kujipima”amesema.

Nakuongeza kuwa
“Sisi sote tunaishi huko mtaani na tunaona tatizo hili lilivyo kubwa na ndio maana Mimi Kila siku nasema kuwa nitasema kweli daima na hapa lazima TANESCO wajipime kwani mara nyingi hatua zinachukuliwa Kwa wanasiasa tu na hivi tutaangalia na uwajibikaji wa watendaji wetu.”amessitiza

Amesema kuwa Chama cha Mapinduzi kinaelekea kwenye chaguzi mwaka ujao na hakitamuonea mtu haya na hakitakuwa tayarii kumvumilia mtu mzembe hivyo lazima wajipime kama kweli wanafanya kazi walizotumwa.

Makonda amesema kuwa watendaji walioko Serikali hawamtendei haki Mwenyekiti wa chama hicho ambaye pia ndio Rais wa Jamhuri wa muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan na ndio maana analazimika kuvunja hadi bodi wakati Yeye alitakiwa alale usingizi.

“Chama hakifurahii hali ya umeme inayoendelea huko mtaani nivema Sasa watendaji walioko kwenye sekta ya umeme kuangalia ufanisi wa kazi zao na kujitatjimini upya.”amesema

Nakuonge kuwa “tatizo la umeme si la Waziri mwenye dhamana tu bali ni la watalamu wote na tunaimani kubwa kwamba kuazia januari 2024 kama tulivyoarifiwa kwamba kinu cha kwanza cha kufua umeme kitaaza kuwashwa mwezi januari hivyo nimatarajia makubwa kwamba tataizo la umeme linakwenda kupungua.

Wakati huohuo Makonda ametumia mkutano huo kutangaza awamu ya pili ya ziara zake za kusikiliza kero za wananchi ambapo amewataka watendaji huko atakakopita kujiandaa vizuri kujibu hoja zitazokawasolishwa na wananchi.

Amesema ziara hiyo itaaza januari 15 katika mikoa ya pwani ,Tanga, Kilimanjaro ,Arusha ,Manyara ,singida ,Tabora ,shinyanga ,pamoja itilima mkoani Simiyu.

Akizungumzia kuhusu utekelezaji wa ilani ya chama hicho ya mwaka 2020_2025 amesema CCM hawana wasiwasi kwani Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika kipindi cha miaka miwili amefanya kazi kubwa na wananchi wanamuunga mkono na hakuna shaka Chama hicho kitafanya vizuri katika chaguzi zijazo.

“Natoa wito kwa Watanzania kujitokeza kushiriki na kutoa maoni yao katika Dira ya Maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 -2050 ili kuchagua Tanzania wanayoitaka”alisema

Amesema kuwa mchakato wa kutoa taarifa kwa vyombo vya habari utakuwa ukifanyika kila baada ya robo mwaka ili kutoa fursa kwa wanaccm na wananchi kufahamu yaliyotekelezwa,baada ya ziara za viongozi wao.

“Tunashukuru baada ya kufanya ziara katika mikoa mbalimbali nchini tija imeanza kuonekana baada ya waziri wetu wa Ardhi Nyumba na Makazi, Jerry Silaa amefanya kazi bora ambayo kwetu CCM ni ya kujivunia baada ya kutatua migogoro mkoani na Dodoma na kuwaondosha watendaji 15 waliobainika kuhusika na migogoro hiyo,” amesema.

“Mwaka huu unaofikia tamati siku chache zijazo watumishi wote wa Serikali wajitathimini kama wameweza kumsaidia Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kiutendaji na ikifika Januari, 2024,wawe wamepata majibu ya kuamua kama wanafaha au la katika nafasi hizo.