1. “Naota mambo yajayo, kwamba siku moja watoto wangu wanne watakaa katika nchi ambayo hawatapambanuliwa kwa sababu ya rangi yao bali kwa sababu ya tabia na mwenendo wao” Maneno hayo yalipata kunenwa na Matin Luther King Junior, mwaka 1963.
 
Mandela: Umoja ni nguvu
2. “Ukitaka kutembea haraka tembea mwenyewe, lakini ukitaka kutembea umbali mrefu basi tembea na watu”  haya ni maneno ya hayati Nelson Mandela Rais wa kwanza mzalendo mweusi wa Afrika kusini.
Lincolin: Serikali ya watu
3. “Serikali ya watu, inayowatumikia watu na iliyowekwa na watu haitopotea duniani,” maneno hayo yalisemwa na  Rais wa 16 wa Marekani,  Abrahamu Lincoln.
 
Papa Yohane Paulo I: Kusoma
 4. “Kama mtu fulani angeniambia kuwa siku moja ntakuwa Papa, ningesoma kwa bidii” haya maneno aliyasema Papa Yohane Paul I enzi za uhai wake.

By Jamhuri