Na Tatu Saad, JAMHURI MEDIA

Baada ya kuondoka jijini Dar es Salaam jumatatu ya Machi 20 mwaka huu mshambuliaji wa klabu ya Yanga Fiston Mayele amesema hatarudi tena Tanzania baada ya kumaliza mchezo wao wa kufuzu AFCON dhidi ya Mauritania.

DR Congo inajiandaa na mchezo huo utakaopigwa Ijumaa ya Machi 24 mwaka huu katika uwanja wa sjapona mjini Douala nchini Cameroon, kisha kurudiana Machi 29 katika uwanja wa Stade Cheikha pilt Boidiya mjini Nouwkchott.

Mayele amesema ameshazungumza na uongozi wa klabu ya Yanga Sc na kukubaliana abaki nchini DR Congo akiisubiri timu hiyo inayoelekea huko kupapatuana na Tp Mazembe.

Amesema maamuzi hayo yamekuja kutokana na ratatiba ya mchezo ujao wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ambao watakuwa nyumbani mjini Lubumbashi mapema mwezi ujao.

“Tunakutana na TP Mazembe Aprili 2 na mimi nitakuwa na mchezo wa marudiano na Mouritania ugenini Machi 28, nitarudi nyumbani DR Congo na timu baada ya mchezo wetu wa pili na Mauritania. Hivyo nitaungana na wenzangu huku.”amesema Mayele.

Mayele amesema suala la kuwa mchezo kukamilisha ratiba ni la mashabiki lakini wao kama wachezaji wamejipanga vizuri ili kuifanya timu iendelee kuongiza kundi.

“Suala la kwamba ni mchezo wa kukamilisha ratiba linabaki kwa mashabiki sisi kama wachezaji tunakwenda kupambana kuhakikisha tunapata matokeo ya ushindi ili kuendelea kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuongoza kundi.” Amesema Mayele

Amesema anaiheshimu TP Mazembe na hawataingia kwenye mchezo huo kwa kujiamini kutokana na matokeo waliyoyapata katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, hivyo wenyeji wao watahitaji kulipa kisasi na kutunza heshima ya kushinda nyumbani kwao.
Young Africans inaongoza msimamo wa Kundi D, Kombe la Shirikisho Barani Afrika ikiwa na alama 10 sawa na US Monastir iliyozidiwa tofauti ya mabao ya kufungana kufungwa.

TP Mazembe inaburuza mkia wa Kundi hilo ikiwa na alama 03, ikitanguliwa na AS Real Bamako inayoshika nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 05.

By Jamhuri