Na Tatu Saad,JAMHURI MEDIA

Uongozi wa Yanga Sc umesema upo tayari kuona kikosi chao kikipangwa na timu yoyote katika hatua ya robo fainali ya kombe la Shirikisho Barani Afrika.

Afisa Habari wa klabu ya Yanga ‘Ali Kamwe amesema kwa ubora wa kikosi cha timu hiyo, hawana hofu ya kukutana na timu yoyote katika michuano hiyo.

“Kwa kikosi chetu cha sasa, hakuna timu kwa Afrika ambayo tunaihofia ila kwa sasa wapinzani wetu ambao wanakuja wanatuhofia.” amesema Kamwe.

“Sisi hakuna timu Afrika kwenye Kombe la Shirikisho ambayo tunaihofia, hata US Monastir walikuwa wanatuhofia, ASEC, Rivers, Pyramids wote wanatuwaza.” amesema Kamwe.

Yanga imetoa tambo hizo baada ya kushinda mechi zote katika ardhi ya nyumbani na kujihakikishia kucheza robo fainali baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya US Monastir Mnamo Machi 19 mwaka huu katika dimba la mkapa jijini Da Es Salaam.

Hata hivyo Ali Kamwe amesema watamalizana na yeyote na watafanya vizuri katika hatua ya robo fainali na kutinga hatua ya nusu fainali.

“Yoyote anayekuja sisi tunamalizana naye na tunaamini kwamba kwenye hatua ya robo fainali tutafanya vizuri na kutinga hatua ya nusu fainali.” Amesema Ally Kamwe.

Kwa sasa Young Africans inaongoza Kundi D na inaweza kukutana na Marumo Gallants (Afrika Kusini), USM Alger (Algeria), Saint-Éloi Lupopo (DR Congo) au Al Akhdar (Libya) zilizopo Kundi A, za Kundi B ni Rivers United (Nigeria) na ASEC Mimosas (Ivory Coast) au zile za Kundi Kundi C, ASFAR (Morocco), Pyramids na Future (Misri).

By Jamhuri