Na Tatu Saad, JAMHURI MEDIA

Wababe wa Soka la Bongo kwa upande wa Wanawake Simba Queens na Yanga Princess kesho Jumatano (Machi 22) wataingia dimbani kupapatuana katika mchezo wa ligi kuu ya wanawake Tanzania.

Katika mchezo huo Yanga Princess watakua wenyeji wakiwakaribisha dimbani Simba Queens ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya wanwake Tanzania.

Yanga SC inaingia mchezoni ikiwa na shauku ya kutengeneza rekodi ya kuwafunga Simba Queens kwa mara nyingine kwenye misimu ya hivi karibuni.

Miamba hii miwili ya soka la wanawake Tanzania walitoka sare ya 1-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu ya wanwake Tanzania katika uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Katika mchezo huu Yanga wana uhitaji mkubwa wa kushinda ili kujitengenezea nafasi kubwa ya kuchukua ubingwa wa msimu huu.

Mpaka sasa Yanga Princess wamepitwa alama tano na Simba Queens wote wakicheza michezo 11 ya mzunguko wa ligi huku wakitoka kuvuna alama moja katika mchezo wao wa mwisho wa ugenini dhidi ya Mkwawa Queens.

Yanga Princess wamekusanya alama 21 kwenye michezo 11 waliocheza, wakati Simba Queens wamevuna alama 26 kwenye michezo 11 ikilingana na Fountain Gate na JKT Queens zenye alama 25 kila moja.

By Jamhuri