Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Mwanza

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linamshikilia Rogers Sunday (41), mpiga debe Kituo cha Mabasi Usagara na mkazi wa Usagara wilayani Misungwi mkoani Mwanza,kwa tuhuma ya kumuingilia kuku hadi kumuua kwa lengo la kujiridhisha kimwili.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Wilbroad Mutafungwa, ameeleza kuwa mtuhumiwa huyo alifanya kitendo hicho Aprili 12, mwaka huu, majira ya saa 6 , katika kijiji na Kata ya Usagara wilayani humo.

“Tukio limetendeka sebuleni kwenye nyumba ya dada yake mtuhumiwa na kushuhudiwa na mtoto wa kike wa dada yake ambaye alikuwepo hapo nyumbani,bado tunachunguza chanzo cha tukio hilo pamoja na kuchunguza afya yake ya akili,” amesema.

Katika tukio lingine, Kamanda Mutafungwa amesema linamshikilia Jackson Kalamaji, mkazi wa Wilaya ya Sengerema kwa kosa la kumchoma kisu mke wake Mariam Bulacha.

Kamanda amesema kuwa tukio hilo lilitokea ambalo lilitokea Aprili 13, mwaka huu, muda wa saa moja usiku.

Amesema Kalamaji alimchoma kisu mke wake kwa kumuhisi kuwa ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine.

By Jamhuri