Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Dorothy Semu amemteua Makamu Mwenyekiti Bara wa chama hicho, Isihaka Mchinjita kuwa Waziri Mkuu Kivuli ACT Wazalendo.

Uteuzi huo umejiri leo Machi 20, 2024 wakati Dorothy Semu alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu kuunda Baraza Jipya la Mawaziri Vivuli la ACT Wazalendo.

Mchinjita amemshukuru Dorothy Semu kwa kumuamini katika nafasi ya Waziri Mkuu Kivuli katika Baraza Kivuli la Mawaziri wa ACT Wazalendo.

“Nabeba wajibu huu wa kuendelea kuwasemea Watanzania na kutoa sera mbadala”, amesema Mchinjita.

By Jamhuri