Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Dar es Salaam

Mchekeshaji anayefahamika zaidi kwa jina la Mzee wa Mjegeje amefariki dunia usiku wa kuamkia leo katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dar es Salaam.

Jamhuri Media imezungumza na meneja wake ambaye amethibitisha kifo chake amesema kuwa marehwmu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa figo, ini na bandama kufeli na damu kupungua.

“Mzee Mjegeje alilazwa Hospitali ya Mwanayamala kwa takribani wiki moja, kwa sasa mwili umetolewa monchwari na mazishi yanatarajia kufanyika nyumbani kwao Keko jijini Dar es Salaam” amesema.

Mzee Mjegeje alijipatia umaarufu mkubwa kwenye mitandao ya kijamii kufuatia misemo yake mbalimbali na vichekesho ambavyo vilimpa fursa mbalimbali ikiwemo makampuni kumtumia kwenye matangazo.