Na Ashrack Miraji, JamhuriMedia, Same Kilimanjaro

Maneja wa RUWASA wilayani Moshi, Mussa Msangi, ametoa agizo la kuuundwa kwa kamati mpya ya maji ndani ya siku saba katika Kijiji cha Singa kufuatia malalamiko ya wananchi kuhusu maji.

Meneja Msangi ametoa agizo baada ya kuhudhuria kwenye kikao cha ndani kilicho fanyika katika ofisi ya Kijiji Cha Singa Wilayani Moshi Mkoani Kilimanjaro kilichohudhuriwa na wenyeviti na wajumbe wa vitongoji vinne vya Singa Chini,Kati,Kifueni na Singa Juu.

Awali wananchi walilalamika kuwa viongozi wao wa vijiji wanahujumu miradi ya maji kwa kutokutoa taarifa sahihi za huduma ya maji na kung’ang’ania nafasi zao kwa maslahi binafsi.

“Kwa muda mrefu, wananchi wa Singa wamekabiliwa na shida ya upatikanaji wa maji kutokana na hali hii. Mkuu wa wilaya aliagiza kamati ya maji iundwe, lakini hadi sasa agizo hilo halijatekelezwa,” amesema Msangi

Ameongeza kuwa “Kwa hiyo, naagiza ofisi ya kijiji itoe semina kwa vitongoji vyote vinne ndani ya siku mbili na kisha kuitisha mkutano mkuu ili kuchagua viongozi watakaoshirikiana na bodi ya Maji katika kuwahudumia wananchi hususani upande wa maji.”

Msangi, amesisitiza umuhimu wa huduma ya maji kwa wananchi na kuhakikisha kuwa maji yanatakiwa yapatikane katika vijiji vyote, ikiwemo Singa.

Pia, ameagiza kamati mpya itakayoudwa lengo ni kuhakikisha wananchi wa Singa wanapata maji na kupewa taarifa mapema kuhusu matengenezo ya miundombinu ya maji.

Wakati huohuo Mwenyekiti wa Kijiji cha Singa, Aloyce Chuwa, ameahidi kuitisha mkutano wa vitongoji ili kuwapa semina wananchi watakaoteuliwa kuwa wanakamati wa maji katika uchaguzi Mkuu utaofanyika Machi 18,2024 katika ofisi ya Kijiji Cha Singa.

“wanakijiji wa Singa lazima tuwe na umoja na kushirikiana katika kuteuwa kamati mpya ya Maji hivyo tujitokeze Kwa wingi katika semina ya uchaguzi wa kwanza na Mkutano Mkuu pia nitakuwa mchoyo wa fadhira nisipo washukuru wadau wa maendeleo kijiji kwetu” amesema Chuwa.

By Jamhuri