Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Sophia Mjema leo ameongoza shughuli ya kuaga miili ya watoto watatu wasioona waliofariki kwa  ajali ya moto ulioteketeza bweni katika shule ya msingi Buhangija Manispaa ya Shinyanga na kusababisha vifo vya watoto hao.

Shughuli ya kuaga miili ya watoto hao imefanyika katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo viongozi wa Dini , wa serikali, viongozi wa chama cha mapinduzi CCM pamoja na wananchi.

Akizungumza kwenye shuguli hilo RC Mjema ameendelea kutoa pole kwa familia zilizopatwa na msiba ambapo amesema kuwa serikali inaendelea na uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.

“Kwanza kabisa naomba nitoe pole nyingi sana kwa familia kwa kupotelewa na watoto wetu hawa ambao tulikuwa tunawategemea sana katika maisha kuona kwamba badae watakuja kuwa watu wambao watasaidia familia lakini yote ni mipango ya Mungu tuipokee kwahiyo tunaomba tutoe pole nyingi sana”

“Jambo hilo limefanyika serikali bado inaendelea kufanya kazi yake ya kuweza kubaini chanzo kilichotokea ni nini ili jambo hili liziweza kutokea tena hasa katika maeneo ya watoto wetu wanaoishi kwenye mabweni”.amesema RC Mjema

Akizungumza kwa niamba ya chama cha mapinduzi CCM Mwenyekiti wa chama hicho Wilaya  wa Shinyanga vijijini  Bwana Edward Ngelela wakati akitoa pole amesema katika kipindi hiki kila mmoja anapaswa kumtanguliza Mwenyezi Mungu.

Zinazohusiana

-Moto wateketeza bweni, waua watoto wenye ulemavu watatu Shinyanga

Usiku wa kuamkia jana Novemba 23,2022 bweni wanalolala wanafunzi wa kike wenye ulemavu liliungua moto na kusababisha vifo vya watoto watatu ambao miili yao imeagwa leo kiserikali.

Waliofariki Dunia ni Miirium Limbu ambaye mwili wake umesafirishwa kwenda Wilayani Kishapu mahali alipozaliwa, Catherine Paulo mwenye mika 10 ambaye mwili wake umesafirishwa kwenda Wilaya ya Maswa Mkoani Simiyu na Caren Mayenga mwenye miaka 9 ambaye amesafirishwa kwenda wilayani  Itilima Mkoani Simiyu.

By Jamhuri