Mkaguzi Kata Iragua, Mkaguzi wa Polisi (INSP) Ramadhan Abdalla, akitoa msaada na maelekezo kwa watumiaji wa barabara katika eneo la Nyanya, Wilaya ya Ulanga, Mkoa wa Morogoro, kufuatia changamoto ya upitikaji wa barabara ili kutokuleta madhara kwa vyombo vta usafiri na watumiaji wengine wa Barabara.
Mkaguzi huyo amewaomba wananchi wanaotumia barabara hiyo, kuendelea kuchukua tahadhari huku akiwasisitiza kuchukua tahadhari ili kuepuka madhara yanayoweza kujitokeza, hasa kutokana na hali mvua zinazoendelea kunyesha.
Ameshauri kuwa, pindi mvua zinapokuwa kubwa, ni vyema watumiaji wa barabara kusubiri hadi mvua zipungue ndipo waendelee na safari zao, ili kuepuka ajali na hatari nyinginezo.
Aidha, amewataka wananchi kuendelea kuwa waangalifu na kufuata maelekezo yanayotolewa na askari wa usalama Barabarani kipindi hiki cha masika, ili kulinda usalama wa vyombo vyao na watumiaji wengine wa Barabara.




