Dar es Salaam

Na Mwl. Paulo Mapunda

Wiki iliyopita tuliwatazama Wapythagoras na ufahamu wao kuhusu ukuu na utukufu wa namba, kwamba kwao 10 ni namba takatifu kwa kuwa ni jumla ya namba moja hadi nne (1+2+3+4=10) na kwamba ni Albert Pike ndiye aliyeweka mpangilio huo ndani ya Msahafu wa Kimasonic (Morals and Dogma), Adam, W akaweka mpangilio huo ndani ya kitabu cha waliovuviwa (Codex Gigas or Satanic Bible). Tuendelee… 

Wakati wa uumbaji zilipita saa 144 hadi Mungu alipomuumba Adamu; yaani siku ya sita. Kwa Wapaithagoras sita humaanisha ‘mtu’, haki ni namba kipeuo cha pili na ndoa ni namba tano. 

Ilipita miaka 300 tangu kuumbwa Adamu hadi Hawa. Zile zinazotajwa kama siku saba za uumbaji na mapumziko kwa Mungu ni sawa na miaka 7,000 kwa binadamu.

Saa 144 ni sawa na 1+4+4=9, lakini ukichukua sita (siku aliyoumbwa Adamu ukajumlisha na tatu jumla ni tisa (6+3+0+0=9). Yesu alikamatwa siku ya tano ya juma na kiroho alihukumiwa siku hiyo hiyo usiku kwa kuwa hata mtu kiroho aliumbwa siku ya tano (Mwz. 1:26,27), lakini kimwili alihukumiwa siku ya sita, kwa kuwa hata mtu kimwili aliumbwa siku ya sita, aliangikwa msalabani saa sita kamili mchana hadi saa tisa alipokata roho, hivyo alihangaika msalabani kwa saa tatu, alilala kaburini siku tatu sawa na saa 72, yaani 7+2=9.

Ukichukua tisa ya jumla ya saa za uumbaji wa mtu (1+4+4) ukijumlisha na tisa itokanayo na siku na miaka ya ukamilifu wake katika muunganiko; yaani uumbwaji wa Hawa ambao unarejesha ukamilifu wa Adamu wa kwanza, kwa kuwa Hawa aliumbwa kwa kufanyiwa ‘operesheni’ Adamu (6+3+0+0=9), ukijumlisha na tisa ya saa (muda) aliokufa Yesu msalabani pale Kalvari, ukijumlisha na tisa jumla ya namba ya saa alizolala Yesu kaburini yaani 7+2=9, unapata thelathini na sita, ambayo ni sawa na 3+6=9, pia ni uficho wa 666 kwa kuwa jumla ya 1 hadi 36, yaani (1+2+3+4+5+6+…36=666. Lakini hata ukichukua jumla ya 1 hadi 9 ni sawa na 45 ambayo ni uficho wa 9 kwa mantiki ya 4+5=9.

Katika kuitukuza namba 36, Wababulonia, watu wa Mesopotamia (au Babeli ya Nimrod, Nebukadreza, Nibonidus na Belshaza) walikuwa na miungu 36 waliyoiabudu, kama mungu jua, mwezi, Ishtar (mwenye wivu; Easter; ‘Passover au Pa’saka’), na miungu mingine mingi.

Shetani ameiga tabia ya Mungu ya kutumia namba ila kwa kinyume ili kuleta uharibifu, kwa mfano kwa Masons, namba moja huwakilisha Mungu muumbaji, lakini kwao namba 11 ni takatifu zaidi kwa kuwa jumla yake ni 2, yaani 1+1, kumaanisha miungu wawili, ukiongeza 1 mbele yake, yaani 111 hutengeneza namba yenye nguvu kubwa zaidi kwa kuwa ikizidishwa na namba yoyote huleta zao la namba hiyo, mfano 111×1=111, 111×2=222, 111×3=333, hivyo inapozidishwa na 6 yaani 111×6=666. 

Wamasonia wameunda jedwali la namba lijulikanalo kama ‘6×6 Matrx’ ambalo ukizidisha namba kwa wima au ulalo au diagonal unapata jumla 666, katika jedwali hilo matukio yote ya uovu yamepangwa kwa kufuata mpangilio wa kiwelevu sana na akili kubwa wa namba zilizo ndani ya jedwali hilo.

Dunia na viijazavyo ni mali ya Bwana, hata namba ni zake bali shetani huzitumia kufanikisha mipango yake miovu. Zipo namba anazopenda kuzitumia katika matukio mbalimbali hususan inapotokea kuna mfuatano wa namba hizo katika tarehe, muda, siku, wiki, mwezi na mwaka kwa kuwa baraka na laana vimefungwa katika muda (nyakati). 

Mathalani namba zifuatazo zinapoongozana kwa mrudio, basi kuwa makini sana; 2,3,5,6,9,11,13,15,17,18,22,23,24,27,29,33,36 orodha ni ndefu, 11 ni uficho wa 2, vilevile 9 ni uficho wa namba 6 ilhali namba 13 ni namba ya uasi kwa msingi wa Mwz. 14:4. 

Lakini itoshe kusema kwamba namba hizo zitumikazo katika kuleta uharibifu (maangamizi), si za kishetani bali yeye hupenda kuzitumia kuleta nguvu katika matukio yake.

Hata kuelekea Pasaka Kuu, siku ya kalamu ya mwisho pale katika chumba cha juu (upper room) kulikuwa na jumla ya watu 13 (Yesu na wanafunzi 12), baadaye wakafa watu wawili; Yesu na Yuda Iskariote, namba ikabadilika na kuwa 11 ambayo ni sawa na 2 kwa maana ya 1+1 =2 sawa na idadi ya watu waliokufa.

Digrii ya juu kabisa kwa waabudu shetani ni 33, iko hivyo kwa kuwa umri alioishi Yesu hapa duniani ni miaka 33 (sawa na 6, yaani 3+3), hata shughuli au vitendo vingi vya kishetani hufanyika usiku, hasa kuanzia saa 6 hadi saa 9 usiku, huo ndio muda ambao Yesu alikuwa ameangikwa msalabani japo ilikuwa ni mchana, lakini kanuni ya wafanya waelewe kinyume ndiyo itendayo kazi kuleta nguvu katika matukio hayo, hivyo kuwa na matokeo makubwa kwa utawala wa kishetani. 

Usiku ni muda wenye nguvu sana kwa shetani na ndiyo maana anaitwa ‘mfalme wa giza’.

Uamuzi wote uletao mabadiliko au uongozao ulimwengu, hutolewa usiku katika vikao vya siri na kunapokucha huwa ni kuhalalisha kile kilichokwisha kupitishwa. 

Hata Yesu alihukumiwa usiku, Ponsio Pilato alihalalisha tu hukumu iliyokwishatolewa na Kayafa usiku wa kabla ya siku ya hukumu iliyokuwa ya kimwili ilhali hukumu ya kiroho ilikwisha kufanywa na Kuhani Mkuu Kayafa akishirikiana na Anasi, mkwewe.

Maandiko yanasema mtaijua ile kweli nayo hiyo kweli itawaweka huru (Yohana 8:32). Mtawala wa ulimwengu huu ambaye ndiye muasisi wa majanga yote yampatayo binadamu, aliweka mipango yake ya uaharibifu katika makundi matano.

Mosi, kwa kutumia vita ambayo ilipangwa kuwa tatu; mbili imekwisha kushuhudiwa (Vita ya Kwanza na ya Pili ya Dunia). Kwa mujibu wa Albert Pike, mwandishi wa Msahafu wa Kimasonia wa ‘Morals and Dogma’ bado vita moja ambayo ni ya mwisho kwa mpangilio waliojiwekea kuelekea mfumo mpya wa ulimwengu.

Pili, ugaidi ambapo tunashuhudia kuzaliwa kwa vikundi vya kigaidi na magaidi duniani kote. Wanateka nyara, wanaua, wanaharibu mali na kutowesha amani ya dunia, vikundi kama IS, Boko Haram, Al Quida, Taliban (kuvitaja kwa uchache) vina mafungamano na watawala wa ulimwengu ili kutimiza ajenda ovu za kumuangamiza binadamu. 

Vikundi hivi vinaasisi machafuko na kuzidhoofisha serikali nyingi duniani. Uchumi wa mataifa umekuwa ukilegalea kutokana na kupambana na vikundi hivi ama kwa kujua au kutokujua siri ya uwepo wake na chanzo cha nguvu za vikundi tajwa. 

Mbali ya kutimiza mipango ya kishetani, pia vinahakikisha GAOTU anakunywa damu inayotiririshwa na magaidi kila kona ya dunia. 

Itakumbukwa kuwa Mungu hakumuumba mtu ili afe bali aiishi apate kuyasimulia matendo makuu, wema, rehema na fadhili za Mungu maishani mwake.

Tatu, uharibifu wa mazingira ili kusababisha ongezeko la joto au baridi duniani. Ongezeko la joto duniani linasababisha barafu kuyeyuka, maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu yanapungua, ukame unaongezeka, hivyo kupunguza malisho kwa wanyama. 

Ongezeko la baridi linasababisha kusambaa kwa haraka magonjwa ya virusi (kama corona) na kusababisha ongezeko kubwa la waathirika na vifo.

Nne, ongezeko la ukiukwaji wa maadili, kuvunjika kwa ndoa, ongezeko la ndoa za jinsia moja, uharibuji wa mimba, ongezeko la matumizi ya dawa za kulevya, kudorora kwa utu, ongezeko la umalaya duniani (ngono za vikundi, ngono za kimfumo), watu kujipenda zaidi kuliko kuwapenda wengine, tofauti na yaagizavyo maandiko (Mathayo 7:12), ongezeko la ndoa za watu na wanyama, watu kutembea uchi au kuvaa nusu uchi na matukio mengine yafananayo na hayo.

Tano, utengenezaji na usambazaji wa vimelea vya kibaiolojia, ili kupunguza idadi ya watu duniani tofauti na agizo la Mungu (Mwz.1:28), mlipuko wa magonjwa ni utekelezaji wa mpango wa kupunguza idadi ya watu. 

Tuwasiliane: [email protected]; 0755 671 071.

By Jamhuri