Na David John,JamhuriMedia

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Karagwe Michael Nzyungu akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake (hawapo pichani) kuhusu maendeleo ya halmashauri hiyo..

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmadhauri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera Michael Nzyungu amempongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye halmashauri hiyo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule mbalimbali za sekondari pamoja na ukamilishaji wa majengo katika hospitali ya Wilaya ya Karagwe.

Amesema moja ya fedha hizo shilingi bilioni 1.32 zimeelekezwa kwa ajili ya kutekeleza wa ujenzi wa vyumba vya madarasa 66 kwa mwaka huu wa fedha ndani ya Wilaya ya Karagwe ambapo lengo kuu ni maandalizi ya kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza mwaka 2023.

Nzuyungu ameyabainisha leo Desemba 7, mwaka hu,u alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake ambapo amefafanua kuwa shule mojawapo iliyopewa fedha ni shule ya Sekondari Rugu iliyopo kitongoji cha Nyakahanga Kijiji cha Rugu wilayani humo kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa.

Amesema kuwa madarasa yote 66 yapo kwenye hatua tofauti tofauti za kuezeka na umaliziaji na hatimaye baada ya muda mfupi madarasa yote yatakuwa yamekamilika, kwa Halmashauri nzima.
Nzuyungu amesema wananchi wa Karagwew wanamshukuru sana Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kuwapa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo wilayani humo.

Vilevile mkurugenzi huyo wa Halmashauri ameongeza kuwa kwa upande wa sekta ya afya, ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ni kubwa ina majengo mengi makubwa na ya kisasa jambo ambalo Halmashauri hiyo inajivunia mradi huo mkubwa na wa kimkakati.

“Tunamshukuru Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha hizo na kwamba fedha hizi zimeletwa kwa awamu nne awamu ya kwanza Halmashauri ilipokea kiasi cha shilingi Bilioni 1.3 kwa yale majengo waliyoelekezwa Halmashauri iliongeza kiasi cha shilingi milioni 300.

“Kwa hiyo awamu ya kwanza ina majengo saba jengo la Utawala, OPD, maabara, exray, wodi ya wazazi pamoja na mambo mengine ambayo yalitumia kiasi cha shilingi Bilioni 1.8, na Bilioni 1.5 zilikuwa za Serikali Kuu na Halmashauri ikatoa milioni 300, hiyo ilikuwa ni awamu ya kwanza 2001,” amesema.

Amesema Nzuyungu mwaka 2002 walipata awamu ya pili walipata shilingi milioni 500 kwa ajili ya kujenga wodi tatu na zimekamilika kuna wodi ya wanaume, wodi ya wanawake na wodi ya Watoto kwamba kwa fedha hizo hazikukamilika Halmashauri ilichangia kwa kuongeza shilingi milioni 60 na kwa sasa ujenzi wa mashimo ya maji taka unaendelea.

Ameongeza kuwa awamu ya tatu ni fedha za COVID 19 kiasi cha shilingi milioni 340 ambapo shilingi Milioni 90 ilitumika kujenga nyumba ya mtumishi inayofaa kuishi familia mbili tofauti na Milioni 250 ilitumika kujenga jingo la wagonjwa mahututi (ICU) na tayari limeanza kutumika na kama Halmashauri umaliziaji wameongeza shilingi Milioni 40.

Amefafanua kuwa kwa awamu ya nne inayoendelea ni fedha walizopata kipindi cha mwaka jana shilingi milioni 800 mwishoni mwa mwaka huu wa fedha kwa ajili ya kujenga wodi za wanawake, wanaume na chumba cha upasuaji pamoja na chumba cha kuhifadhia maiti na kufafanua kuwa kuna majengo yamekamilika kama mochwari lakini na majengo mengine yanaendelea kukamilika.

“Nachoshukuru Serikali ya Awamu ya Sita imetupendelea sisi Karagwe tuna majengo mengi sana na tunaendelea kupokea vifaa lakini changamoto kubwa uhaba wa watumishi hawatoshi unajua Karagwe ni mbali na tukipata watumishi hawaji wote, changamoto nyingine ni ukosefu wa gari la wagonjwa zilizopo ni mbili moja inatumika wilayani na nyingine kwenye vituo vya afya vijijini,” amesema Mkurugenzi.

Pia mkurugenzi amesema kuwa moja ya miradi wanayotekeleza kwa fedha za ndani ni ujenzi wa stendi ya kisasa ya mabasi ambapo wameingia makubaliano mwekezaji wa ndani na kwamba itakapo kamilika mwekezaji huyo ataimiliki kwa muda wa miaka saba na baada ya hapo itarudi mikononi mwa Halmashauri kwa asilimia 100.

Jengo wagonjwa mahututi lililopo katika hospitali ya Halmashsuri ya Wilaya ya Karagwe mkoani Kagera limejengwa kwa fedha kutoka Serikali Kuu

By Jamhuri