Na Isri Mohamed, JamhuriMedia, Zanzibar


Rais wa shirikisho la soka Afrika (CAF), Patrice Motsepe amekiri kama angekuwa upande wa shabiki angeona goli la Yanga lililokataliwa na mwamuzi katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Mamelod Sundowns Afrika Kusini kuwa lilikuwa goli halali.

Rais Motsepe ameyasema hayo leo alipowasili visiwani Zanzibar katika fainali za African schools football na kupokelewa na mwenyeji wake Rais wa TFF Wallace Karia.

“Ningekuwa shabiki pia ningeona lile lilikua ni goli ila mimi ni Rais siwezi kucomment chochote naacha mamlaka zenye haki zifanye Kazi yake” amesema Motsepe.

“Baada ya Mechi ya Mamelodi na Yanga Kumalizika nilikutana na Rais Karia nilidhani Kama ilikuwa ni goli lakini Rais wa CAF hatakiwi kutoa maoni yake tunatakiwa kuheshim kanuni na sheria za soka na VAR”

Goli hilo lilifungwa na kiungo wa Yanga Stephen Aziz Ki ambapo mwamuzi alilikataa kwa kile alichoamini mpira haukuvuka mstari wa goli.

By Jamhuri