Makamu wa Rais Dk Philip Mpango amewataka vijana wanaosoma katika vyuo vya ufundi stadi kutumia ujuzi walioupata kutengeneza fursa ya ajira.

Dk Mpango ameyasema hayo wakati akiweka Jiwe la Msingi katika chuo cha ufundi stadi kilichopo kata ya Kasera Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Amesema uwepo wa vyuo hivyo utumike katika kuzalisha na kutengeneza fursa za ajira sambamba na wataalamu ambao wataweza kusaidia kuiletea nchi yetu maendeleo.

Hivyo ili kuwaongezea umahiri vijana wanaopatiwa mafunzo na vyuo hivyo Makamu wa Rais amezitaka sekta binafsi nchini kutoa nafasi za mafunzo ya vitendo Kwa vijana hao kwenye maeneo yao Ili waweze kuwamahiri kwenye fani walizozisomea.

Chuo cha Veta Mkinga ujenzi wake umemtuma takribani Sh bilioni 2 na kina uwezo wa kudahili wanafunzi zaidi ya 240 wa fani mbalimbali.