Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia
BOHARI ya Dawa (MSD) imewashika mkono watoto wanaolelea katika kituo cha kulelea watoto Kurasini kwa kuwapa zawadi mbalimbali kusherehekea sikukuu ya Krrismas na mwaka mpya.
Akizungumza jana kituoni hapo wakati wa kukabidhi msaada huo, Meneja Mawasiliano na Uhusiano MSD, Eti Kusiluka amesema katika kipindi hiki cha sikukuu ya Krismas na mwaka mpya bohari hiyo imeona kuna haja ya kufurahi na watoto hao kwa kuwapelekea zawadi ya sikukuu.
“Sisi ni wazazi na watoto hawa na wana haki ya kufurahia kwa hiyo tumekuja na dawa za miswaki 400, mchele kilo 300, maharage kilo 100, unga kilo 300 ,vitu vya shule kama daftari, penseli, mafuta, sabuni ya unga, sabuni ya kuogea, mafuta pamoja na zawadi nyingie ndogondogo.
“Mbali na zawadi hizo tumekuja na bidhaa ambayo tumeitoa kwenye ghala letu la MSD ya magodoro 80 .Hivyo zawadi zote za sikukuu pamoja na vifaa vya shule ambavyo tumekabidhi vinagharimu Sh.milioni 17.MSD imetoa zawadi kwa watoto hao ili nao wajisikie na kufurahia, tunaamini ni watoto wanaohitaji furaha kama watoto wengine,” alisema.
Meneja wa MSD Kanda ya Dar es Salaam Betie Kaema, ameiema uamuzi wa kuunga na watoto hao unalenga kufurahi nao kama wanavyofurahi na watoto wao walioko nyumbani.
“MSD tumeamua kuja kwa kufurahi na watoto hawa , na hii si mara ya kwanza kuja kuwaona, tumekuwa tukifanya hivyo mara kadhaa. Sisi ndio mama zao, ndio baba zao kwa hiyo tumekuja kuwapa kidogo tulichonacho ili furaha yao itimie,” ameeleza.
Kwa upande wake Ofisa Ustawi wa Jamii Kituo cha Taifa cha kulea watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha Kurasini Farida Ismail, aliihukru MSD kwa kuwapatia zawadi hizo ambazo zitawasaidia katika malezi ya watoto hao.
Amefanua kuwa msaada huo wa MSD unakwenda kunufaisha watoto wapatao 60 wanaolelewa katika kituo hicho huku akitumia nafasi hiyo kutoa rai kwa wadau wengine kusaidia jamii yenye uhitaji ikiwemo ya vituo vinavyolea watoto wanaoishi katika mazingira magumu.
Awalii Mkurugenzi wa TEHAMA na Takwimu kutoka MSD, Leopold Shayo, amesema wametoa msaada huo kama sehemu ya kutekeleza wajibu wa Serikali wa kusaidia wenye uhitaji wakiwemo watoto hao ambao wanalelewa katika kituo hicho.
Zawadi hizo zina thamani ya sh. milioni 17 zikij⁴umuisha mahitaji mbalimbali ya watoto hao vikiwemo vya kula, magodoro na taulo za kike kwa wasichana.