SACP Ng’anzi awataka abiria kutoa taarifa madereva wanaokiuka sheria za barabarani

Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea

Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Tanzania Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi amewataka abiria  wanaosafiri ndani na nje ya Mkoa Ruvuma  kutoa taarifa  za baadhi ya madereva wanaokiuka sheria za usalama barabarini.

Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ng’anzi ameyasema hayo leo wakati alipotembelea kituo kikuu cha mabasi kilichopo eneo la Shule ya Tanga manispaa ya Songea Mkoa wa Ruvuma.

Amesema kuwa huo ni maendeleo wa ziara yake ya ukaguzi wa vyombo vya moyto mkoani humo ambapo amewaonya madereva wenye tabia ya ulevi pamoja na kuendesha magari kwa mwendo kasi na watakaobainika watachukuliwa hatua kali za kisheria ikiwemo ya kunyang’anywa leseni. 

Kamanda wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania SACP Ramadhani Ng’anzi akisoma taarifa ya kipimo cha ulevi kwa mmoja wa madereva wa mabasi ya Superfeo, alipofanya ukaguzi wa mabasi na kupima madereva kiwango cha ulevi.

Pia amewataka madereva wa mabasi kuendesha  kwa kujihami na kuchukua tahadhali wakati wote wawapo safarini ili kulinda usalama wao pamoja na abiria na watumiaji wengine wa barabara wakiwemo watembea kwa miguu.

Aidha amewahimiza madereva wote ambao wanaosafiri kwa umbali mrefu kuhakikisha wanatii sheria za usalama barabarani sambamba na kuachana na matumizi ya  vulevi kwani chanzo cha ajali nyingi husababishwa na sababu nyingi ikiwemo ulevi.

 SACP Ng’anzi kwa kushirikiana na askari wengine wa Kikosi cha Usalama Barabarani walimalizia kazi hiyo  kwa kukagua mifumo mbalimbali ya vidhibiti mwendo vya mabasi ikiwa ni pamoja na mifumo ya breki, Mataili, ubora wa magari  pamoja na  kuwapima ulevi madereva wote  kabla ya kuwaaruhusu kuanza safari zako.

Baadhi ya madereva wa mabasi yaendayo nje ya Mkoa wa Ruvuma na ndani ya Mkoa wakimsikiliza mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Tanzania SACP Ramadhani Ng’anzi.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya usafirishaji wa mabasi ya SuperFeo Abdulab Kisiwa amelishukuru jeshi la polisi kupitia kiasi cha salama barabara kwa kuona umuhimu wa kutembelea mkoani Ruvuma na kufanya ukaguzi wa vyombo vya moto wenye lengo la kupunguza ajari za barabarani jambo ambalo limekuwa ni kero kubwa kwa Jamii.

Awali akimkaribisha mkuu wa kikosi cha usalama barabarani kuzungumza na madereva hao, Mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Ruvuma Issa Milanzi alisema kuwa huu ni muendelezo wa ziara yake ya kukagua vyombo vya moto na kuongea na madereva pamoja na abiria kuhusu kuona kama  wanatumia tiketi za mfumo wa kierektroniki pamoja na kufunga mkanda wawapo safarini.

Kwa upende wao baadhi ya madereva wa mabasi ya abiria wakizungumza wakati zoezi hilo la ukaguzi likiendelea walisema kuwa wamefurahishwa na kitendo cha kukumbushwa umuhimu wa kuzijuwa sheria za usalama barabarani ambazo zitaweza kuepusha kutokea kwa ajari.

SACP Ramadhani Ng’anzi akiwa akizungumza mkuu wa kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Ruvuma Issa Milanzi
Mmoja wa madereva wa mabasi ya Super Feo akipimwa kipimo cha ulevi