NJOMBE, Mvua iliyoambatana na upepo mkali jioni ya tarehe 19/1/2024 imesababisha kaya zaidi ya 20 kukosa makazi kwa kuezua bati la nyumba  na zingine kubomoka katika kata ya Luwumbu, Lupalilo na Mang’oto 

Taasisi kadhaa pia zimekumbwa na maafa hayo ikiwemo kanisa la TAG Luwumbu, kanisa la TAG Ipululu, Ofisi ya chuo Cha Mategemeo Mang’oto na vyumba viwili vya madarasa katika shule ya Sekondari Mango’to

Mkuu wa Wilaya ya Makete Mhe. Juma Sweda  amefika maeneo yaliyopatwa na maafa hayo kuwapa pole na kuwapongeza.Wanajamii kwa ushirikiano walioutoa kwa wenzao walioezuliwa nyumba zao huku akihamasisha kupanda miti ili kuzuia athari zinatokanazo na mvua inayoambatana na upepo 

Diwani Kata ya Luwumbu Mhe. Felix Kyando amesema wananchi wake wameanza kusaidia kupiga bati baadhi ya nyumba zilizoezuliwa na kukusanya michango Iii kununua bati na vifaa vya kusaidia ujenzi  Ili nyumba ambazo zinahitaji ukarabati mkubwa ziweze kurekebishwa huku akiiomba Serikali kuwasaidia pale walipokwama

Kamati ya maafa Wilaya itaenda maeneo yote yaliyopata maafa Ili kutathimi hasara iliyojitokeza ili Serikali iweze kuwasaidia wananchi warudi katika maisha yao ya kila siku.