Naibu Waziri wa Uchukuzi Kihenzile atembelea banda la TPA

Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA limeendelea kuwa kivutio kwa watembeleaji wa maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya Zanzibar yanayoelekea ukingoni.

Mbali na unadhifu wa Banda linalopambwa na picha kubwa za Bandari mbalimbali, kivutio kingine ni mifano ya Meli na Vitendea kazi Bandarini ambavyo vinavutia kundi la Wanafunzi ambao hupenda kuja kwa wingi kujionea operesheni za kibandari zinavyofanyika.

Naibu Waziri wa Uchukuzi David Kihenzile na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA Bw. Masanja Kadogosa, ni miongoni mwa Wageni Maarufu waliotembelea Banda hilo Wiki hii.