Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Unguja

Mwenyekiti Taifa wa Chama cha NCCR – Mageuzi, Haji Ambar Khamis amempongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa kusimamia vyema maadhimisho ya miaka  60  ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa Amani na umoja.

Ameyasema hayo huko wakati akizungumza na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mkoani Unguja.

Amesema, miradi iliyozinduliwa na Serikali ya Dk. Mwinyi katika maadhimisho hayo imedhihirisha kazi kubwa aliyoifanya ya kuwatumikia Wananchi hivyo chama hicho kitaendelea kushirikiana naye ili kuleta maendeleo Nchini.

Hata hivyo amesema chama hicho hakitashiriki Maandamano ya Amani yaliyotangazwa na Chama cha Demikrasia na Maendeleo (CHADEMA) kufanyika  nchini ya  kupinga marekebisho ya sheria ya uchaguzi kwa vile chama hicho kimeshapeleka  mapendekezo yao katika marekebisho hayo.

Amesema maandamano si njia sahihi ya kutafuta muafaka wakati zipo njia mbadala za kutafuta suluhu  pale mnapotofautiana hivyo amewataka wanachama wa chama hicho kutokujihusisha na maandamano hayo.