Na Cresensia Kapinga, JamhuriMedia, Songea.

Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira, vijana na wenye Ulemavu Profesa, Joyce Ndalichako ameonesha kufurahishwa na huduma zinazotolewa na mfuko wa Hifadhi za Jamii (NSSF) mkoani Ruvuma kwani ameshuhudia kuona wanachama wanadai kuwa hawana kero na kwamba ni taasisi chache sana za Serikali na za umma ambazo unaenda kuwasilikiza wanachama, wastaafu na wakasema kuwa hawana kero.

Profesa Ndalichako hayo ameyasema jana wakati akiongea na wafanyakazi, wanachama pamoja na wastaafu wa mfuko huo kwenye viwanja vya ofisi ya hiyo iliyopo Manispaa ya Songea na kwamba amewataka waendele kuboresha NSSF huduma zaidi ili wateja wao waendelee kuiamini NSSF.

Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira vijana na wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza mmoja wa wastaafu wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF leo

Amesema kuwa wengi waliojitokeza kupeleka kero zao, nyingi zinahusiana na waajiri wao na hivyo amewataka kwenda kuwasiliana na waajiri wakiwa na nyaraka zinazoonesha makubaliano kati yao na mwajiri ili kuondoa ukakasi unaweza kujitokeza na si vinginevyo.

” Ni vizuri unavyoenda kwa mwajiri uwe unafahamu je kunamakubaliano hayo maana Kuna mwingine anakuja hapa anasema sijalipwa kiinua mgongo unamuuliza uliahidiwa utalipwa shilingi ngapi anasema sijui, sasa haki yako si unatakiwa uijuwe ndugu zangu kwa sababu sio kila mwajiri ambaye anayetoa kiinua mgongo isipokuwa unapata mafao yako kwenye mifuko kulingana na mchango wako uliyochangia na mshahara wako na wengi waliokuja hapa wamezungumzia swala la kiinua mgongo ambalo haihusiani na NSSF.”amesema Profesa Ndalichako.

Baadhi ya wastaafu wa mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF akitaka kujuwa ufafanuzi

Amesema kuwa toka Jana alipozindua kampeni ya kusikiliza kero za wanachama na wastaafu wa mifuko ya Jamii wengi wao wamekuwa wakitaka kufahanu namna ya kupata kiinua mgongo, kupandishwa cheo, kulipwa mshahara mpya ambapo jambo ambalo amedai kuwa halihusiani kabisa na mifuko ya huduma za Hifadhi za jamii ikiwemo NSSF.

Awali akimkaribisha Mgeni rasmi Waziri wa nchi ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Kazi, Ajira, vijana na wenye Ulemavu Profesa Joyce Ndalichako, Mkurugenzi mwendeshaji wa NSSF Omary Mziya amesema kuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF unamikakati mizuri kwaajiri ya kuhakikisha kuwa huduma zinatolewa kwa wakati na kwamba wateja wanapaswa kuhudumiwa bila kuwepo na malalamiko ya aina yeyote na pale tatizo linapojitokeza hatua zinachukuliwa kwa haraka iwezekanavyo.

Nao baadhi ya wanachama pamoja na wastaafu wameishukuru serikali kwa jinsi mashirika ya Hifadhi ya Jamii yanavyotoa huduma kwa wanachama wake na kwamba utaratibu huo wa kuwasaidia wastaafu wanapohitaji huduma kwa haraka uendelee ili kupunguza malalamiko yanayoweza kujitokeza.