Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) yadaiwa kushindwa kutua kwenye uwanja wa ndege wa Bukoba.

Mbunge wa viti maalumu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Neema Lugangira kupita ukurasa wake katika mtandao wa Twittter amesema amepanda ndege leo asubuhi kuelekea Bukoba lakini safari ilikuwa na changamoto na kwamba wamefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua. Nampongeza Rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba.” Ameandika Lugangira