Serikali imekiri kushilikiwa kwa ndege Airbus A220 tangu Januari kwenye kiwanja cha ndege cha Maastricht Aachen nchini Uholanzi.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk Eliezer Feleshi amesema kuwa ndege inashikiliwa baada ya mwekezaji wa Kiswidi kushinda tuzo ya dola za kimarekani milioni 165 baada ya kuishawishi Mahakama ya Uholanzi kuishikilia ndege ya Tanzania wakati pingamizi ikiendelea.

Mgogoro huo umetokana na kufutwa mpango wa kuendeleza mashamba ya sukari wilayani Bagamoyo ambao ulikuwa na malengo ya kuzalisha sukari kwa ajili ya kuuza nje ya nchi na ethanol ili kuzalishia umeme.

Mradi huo ulipata pingamizi kutoka kwa wanaharakati wa ndani wakiwawakilisha wakulima 1300 ambao bado walikuwa wakitumia ardhi hiyo. Pia mwekezaji huyo aliilaumu Serikali ya Tanzania kushindwa kutengeneza kanuni za sekta ya sukari na kufanya ardhi hiyo kuwa na vikwazo.

Zinazohusiana

Ndege ya ATCL yadaiwa kushindwa kutua Bukoba

Serikali mwaka 2016 ilifuta hati hiyo. Aprili, 2022 Mahakama iliipa ushindi wa tuzo yenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 165 Kampuni ya EcoDevelopment. June 16, ikiwa ni siku moja baada ya ICSID kupokea maombi ya Tanzania kubatilisha hukumu hiyo, Ecodevelopment ilipata ruhusa (leave) kutoka kwenye mahakama ya wilaya ya The Hague kutimiza na maamuzi ya upande mmoja kutoka kwa jaji wa Limburg yaliyotoa kibali cha kuishikilia ndege.

Ndege ya Airbus A220 ilikuwa tayari imenyimwa ruhusa ya kupaa tangu Januari kwenye kiwanja cha ndege cha Maastricht Aachen taarifa ikisema ni kutokana na matatizo kwenye injini.

Undani wa taarifa hii soma HAPA

By Jamhuri