Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewasili katika eneo la Olmoti kwa ajili ya Hafla ya kumkabidhi mkandarasi eneo la ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu Jijini Arusha leo Aprili 6, 2024.

Ndumbaro ameambatana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Jerry Slaaa, Uongozi wa Mkoa wa Arusha, Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Hamis Mwinjuma, Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Elimu, Utamaduni na Michezo wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Mussa Sima, Naibu Katibu Mkuu Dkt. Seleman Serera.

Wengine ni Mkandarasi, Mshauri Elekezi na Viongozi wengine wa Mkoa wa Arusha na Watendaji wa Wizara pamoja na wananchi wa Jijini la Arusha.     

By Jamhuri