Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) Dkt. Tulia Ackson amekutana na kufanya mazungumzo na Viongozi kutoka Benki ya NMB wakiongozwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo, Ndg. Ruth Zaipuna walipomtembelea leo tarehe 7 Novemba, 2023 ofisini kwake jungeni Jijini Dodoma.

Pamoja na mambo mengine viongozi hao wamempongeza Mhe. Spika kwa kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU).

Kwa upande wake Mhe. Spika aliishukuru Benki hiyo kwa kujitoa kwake kulisaidia Bunge katika shughuli mbalimbali hususan michezo.

Shar