Na Cresensia Kapinga, Jamhurimedia, Songea

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Ruvuma, umekabidhi mashuka katika hospitali ya Mkoa wa Ruvuma (HOMSO) yenye thamani ya zaidi ya sh.milioni 1.5 ili kuwasaidia Watanzania na wadau wa mfuko huo watakao lazwa hospitalini hapo na si vinginevyo.

Mashuka hayo yamekabidhiwa hivi karibuni na Meneja wa mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), Mkoa wa Ruvuma Yahya Mudhihiri katika maadhimisho ya wiki ya wadau wa mfuko wa huo ambayo yaliambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo upimaji wa afya kwa wadau wa mfuko huo na watu wengine ambao sio wateja.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Bw.Yahya Mudhihiri akikabidhi msaada wa mashuka kwa mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) Dkt. Magafu Majura.

Alisema kuwa wametoa mashuka hayo kwa lengo la kurudisha shukrani kwa jamii na yatawasaidia wagonjwa wote wakiwemo wateja wa mfuko huo.

“Tunataka wanachama wetu wa mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF)tuendelee kuwapa huduma nzuri hivyo tunatoa msaada huu wa mashuka ili yaweze kuwasaidia watanzania wenzetu na wateja watakao lazwa hapa hospitalini tunaomba mpokee kidogo tulichonacho na tunasema kidogo ni kwa sababu ya idadi ya wagonjwa wanaolazwa hapa HOMSO.”amesema Mudhihiri .

Kwa upande wake mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) Dkt. Magafu Majura ameushukuru mfuko huo wa Taifa wa Hifadhi Jamii (NSSF)kwa kuwapatia msaada wa mashuka hayo kwani utasaidia jamii itakayo kuwa inalazwa hapo na kupunguza uhaba wa mashuka.

Meneja wa mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa wa Ruvuma Bw. Yahya Mudhihiri akimjulia hali mgonjwa .
Baadhi ya wahudimu wa idara ya Afya katika hospital ya Mkoa Songea

By Jamhuri