Mwalimu Nyerere: Tuendeleze 
demokrasia tupate maendeleo

“Jambo kubwa kwa maendeleo ya nchi yetu ni kuendeleza demokrasia yenyewe na siyo muundo unaoiendesha. Jambo hili litakapoletwa ili liamuliwe na mkutano wa Chama, hoja zitakazoongoza uamuzi huo lazima ziwe na uhusiano na hali halisi na mahitaji ya Tanzania ya wakati huo.”

Haya ni maneno ya Baba wa Taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Anna Mkapa: Tuwawezeshe

wanawake wajikwamue

“Mfuko wa Fursa Sawa kwa Wote (EOTF) umekusudia kwa nguvu zake zote kuendeleza juhudi hizi za kuwawezesha wanawake nchini kujikwamua katika wimbi la umaskini, maradhi na ujinga.”

Maneno haya ni ya Anna Mkapa, Mwenyekiti wa EOTF na mke wa Rais mstaafu wa Tanzania, Benjamini William Mkapa.

 

Dk. Shein: Italia inachangia

kuinua uchumi Zanzibar

“Mchango wa wawekezaji kutoka Italia katika uchumi wa Zanzibar, hasa kwenye sekta ya utalii ni mkubwa na umewafanya wananchi wa nchi hizi mbili kuwa karibu.”

Kauli hii ni ya Rais wa Zanzibara na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein.

 

Halima Mdee: Siasa ni

chafu inapoingiliwa

“Siasa inaweza kuwa mchezo mchafu pale inapoingiliwa na watu wenye nia mbaya. Katika mazingira safi ya watu kufanya siasa wakiwa na malengo na nia safi hapo ni vigumu kuona siasa ni mchezo mchafu.”

Haya yalisemwa na Halima Mdee, Mbunge wa Kawe, Dar es Salaam kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).

 

 

1422 Total Views 1 Views Today
||||| 0 I Like It! |||||
Sambaza!