Sehemu ya 7
Kama shule iko kijijini (na katika shule mpya zitakazojengwa siku zijazo)
itawezekana kwamba shamba la shule liwe karibu karibu na shuleyenyewe. Lakini
katika miji na katika shule za zamani zilizo katika vijiji vyetu vyenye watu wengi,
huendaisiwezekane kuwa hivyo.
Katika hali hiyo shule inaweza kutilia mkazo kazi zingine zenye kuleta uchumi, au
inawezekana katika shule za mabweni wanafunzi wakatumia shemu ya mwaka
darasani, na sehemu nyingine katika kambi ya shamba lao lililo mbali.
Kila shule itafanya mpango wake. Itakuwa makosa kuzisamehe shule za mijini,
hata kama watoto huja shule kila siku, wasitimize mpango huu mpya.
Kazi nyingi ambazo wanafanyiwa wanafunzi, hasawale walio katika shule za
Sekondari,zapasa zifanywe na wanafunzi wenyewe. Kwanza, mtoto anayeingia
katika shule akiwa na umri wa miaka saba, atakuwa na umri wa mika 14 akiingia
shule ya Sekondari, na umri wa miaka 20 na 21 amalizapo.
Lakini katika shulezetu nyingi sasa tunajiri shamba boi, siyo kuwafunza watoto
kazi, bali kuifanya kazi ile badala ya watoto wenyewe. Wanafunzi wanakuwa na
mawazo ya kuandaliwa chakula chao na watumishi, na kuoshewa sahani,
kufagiliwa vyumba, na bustani zao kuangaliwa.
Hata kama wakiombwa kusaidia katika kazi hizi wanaona unyonge, na kufanya
kidogo kadri inavyowezekana, na kama mwalimu yupo anawaangalia. Hii ni kwa
sababu hawakujifunza kujivunia chumba safi na bustani nzuri, kama vile
wanavyojivunia insha safi na hesabu walioifanya vizuri.
Lakini je, haiwezekani kazi hizi zikaunganishwa katika jumla ya mafunzo ya
shule? Ni lazima Mwalimu Mkuu na makarani wake watumie muda mrefu
kuandika waranti za kusafiria watoto wakati wa likizo?
Haiwezekani hata moja ya kazi hizi zikafundishwa darasani, ili watoto wajifunze
kufanya kazi hizi wenyewe? Yaani, haiwezekana hata shule za sekondari, zikawa
zinazojitosheleza kiasi chake, ambako waalimu na waangalizi wanaletwa kutoka
sehemu zingine, bali kazi zinginezinafanywa amana na jumuiya nzima ya shule au
kulipiwa gharama ya pamoja? Ni kweli kwamba kwa wanafunzi shule ni mahali pa
kupita tu, lakini hapa ndipo patakapokuwa kwao kwa muda wa miaka saba
mizima.
Ni dhahiri kwamba hali kama hiyo haiwezi kufikiwa kwa siku moja. Kunahitajiwa
mabadiliko makubwa ya mipango na mafunzo, na kwa hiyo mabadiliko hayo
hayana budi kuletwa pole pole madaraka zaidi ya kujitosheleza.
Wala ahaitegemei kwamba watoto wa shule za msingi wanaweza kujitosheleza
sana wenyewe, ingawaje yatupasa kukumbuka kuwa wale wakubwa watakuwa na
umri wa miaka 13 na 14, umri ambao watoto katika nchi nyingi za Ulaya huwa
tayari wanafanya kazi.

Lakini ingawa shule za msingi haziwezi kutarajiwa kujitegemea kama shule za
sekondari, ni muhimu kabisa kwamba shule hizo, na wanafunzi wao, ziwe na
uhusiano kamili na maisha ya vijijini. Wanafunzi lazima waishi kama sehemu ya
jamaa ya uchumi kwa kuwa na wajibu katika jamaa hiyo, na kukifanya kijiji kishiriki
katika mambo ya shule.
Vipindi vya mwaka wa shule, na vipindi vya darasani, vyote vipangwe katika
namna itakayowawezesha wanafunzi, kama watu wa jamii, na watoto wa kijiji,
washiriki kazi katika shamba la jamii la kijiji. Kwa sasa watoto wasiokwenda shule
wanalima shambani kwa baba au katika shamba la ushirika au wanachunga
ng’ombe; hiyo ni lazima kwao.
Yapasa liwe jambo la lazima kwa watoto wanaosoma shule waweze kushiriki kazi
za jamaa, si kwa kupendelewa au kwa hiyari wakati tu wanapotamani kunyoosha
maungo, lakini kama sehemu ya kawaida ya malezi yao.
Mtindo wa sasawa kuihesabu shule kuwa ni kitu cha pekee, na wanafunzi kama
watu wasiolazimika kufanya kazi, hauna budi uachwe. Katika jambo hili wazazi
wana wajibu maalum, lakini shule pia zinaweza kusaidia sana kuunda mawazo
haya mapya.
Kuna njia nyingi tofauti za kuufikia uhusiano huo. Lakini lazima watoto watambue
kwamba wanaelimushwa na umma ili wawe raia wenye akili na bidii kutimiza
wajibu wao katika umma.
Njia moja inayowezekana ya kufanya hivi ni kuleta katika shule za msingi mpango
wa kujifunza kwa vitendo kama vile vile inavyoshauriwa iwe katika shule za
sekondari. Kama watoto wa shule za msingi wanafanya kazi katika shamba la
ushirika la kijiji,tuseme wamegawiwa kipande chao maalum kukiangalia, basi
watajifunza maarifa mapya ya kilimo na kujivunia mafanikio ya shule yao.
Lakini kama hakuna shamba la ushirika kijijini basi shule inaweza kuanzisha
shamba lao wenyewe kwa kuwaomba wale walio wakubwa zaidi wafyeke misitu
wakati watoto wengine wanapofanya kazi nyingine za jumuiya.
Kadhalika iwapo kazi za maendeleo, kama vile majumba mapya na vitu vingine
vinatakiwa katika shule, basi wanafunzi na wakazi wa kijiji washiriki
pamoja,wakigawana kazi zinazolingana na afya na nguvu za kila mmoja wao.
Watoto wa shule, wavulana kwa wasichana, yawapasa waangalie usafi wao
wenyewe, na wajifunze faida ya kufanya kazi pamoja,nay a kuweka mipango ya
maisha ya baadaye. Kwa hiyo, kama wana shamba lao wenyewe, watoto
watahusika katika akzi tu bali vile vile katika ugawaji wa mazao
yanayopatikana,nay a kula nay a kuuza pia.
Hwana budi washiriki katika kuchagua baina ya faida za shule na faida za kijiji, na
baina ya faida za sasa na faida ya baadaye. Kwa njia hizi na zingine watoto
hawana budi, wajifunze tangu mwanzo mpaka mwisho wa mafunzo yao, kwamba
elimu haiwatengi, bali inawasaidia kuwa raia wenye faida katika kijiji, kwa faida
zao wenyewe na kwa faida ya taifa zima nay a nchi zilizo jirani.
Ugumu mmoja wa mpango huu mpya ni mtindo wa sasa wa mitihani. Kama

wanafunzi wanatumia wakati mwingi zaidi wakijifunza kazi za mikono, na katika
kufanya kazi zingine zitakazowasaidia kuwapatia chakula wakati wa masomo yao,
hawataweza kufanya mitihani ya aina ya sasa au katika muda ule ule wa
mafunzo.
Lakini ni vigumu kuelewa kwa nini mtindo wa sasa wa mitihani usibadilishwe. Nchi
zingine zinaanza mtindo huu wa kuchagua wanafunzi wao, ama kwa kuacha
mitihani kabisa toka madarasa ya chini, ama kwa kuchanganya mitihani na njia
nyingine za kupima akili.
Hakuna sababu Tanzania isiunganishe mtihani unayotungwa kufuatana na
mafunzo yanayotolewa, pamoja na makadirio ya mwalimu ya kazi ya mwanafunzi
aliyoifanya kwa ajili ya shule na kwa ajili ya kijiji.
Nji hii ingefaa zaidi kuchagua wale watakaoingia katika shule za sekondari, vyuo
vya ualimu, na vyuo vikuu n.k., kuliko njia ya sasa ya kufaulu mtihani tu. Mpango
kamili wa elimu ya aina mpya utakapokuwa umefanywa, itabidi suala la uchaguzi
wa watoto lichunguzwe tena.
Mpango huu mpya wa kazi katika shule zenu unahitaji mabadiliko makubwa katika
utaratibu wetu. Pengine itaonekana haja vile vile ya kutazama upya jinsi ya
kuugawa mwaka katika vipindi vya shule, na kubadilisha mtindo wa sasa wenye
likizo ndefu ndefu.
Mifugo haiwezi kuachwa peke yake kwa sehemu ya mwaka, wala shambala shule
haliwezi kutoa mazao ya kutosheleza wanafunzi ikiwa wakati wa kupanda,
kuvuna, au wa kupalilia watu wote wako livu.
Lakini inawezekana likizo za shule zikagawanywa ili watoto wa darasa Fulani
waweze kwenda livu wakati wengine wako shule, aum katika shule za sekondari
ambako madarasa yana vikosi viwili viwili, kikosi kimoja kiende livu na kingine
kibaki shuleni. Utaratibu kama huo ni kazi kubwa kuupanga, lakini hakuna sababu
tushindwe ikiwa kweli tumeamua kufanya hivyo.

By Jamhuri