Na Byarugaba Innocent-ORMV

Watumishi wa Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana wameendelea kujiweka sawa kwa mazoezi kabambe ya utimamu wa mwili na viungo Kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Kisasa kufuatili Mashindano ya Shirikisho la Michezo la Wizara na Idara za Serikali,2026 yatakayotimua vumbi Mkoani Kilimanjaro

Uzinduzi wa Mashindano hayo unatarajiwa kufanyika tarehe 25 Septemba,2026 na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba

Aidha,lengo la Mashindano haya ni kuwakutanisha watumishi wa Umma ili kuimarisha afya na kujenga Mahusiano mazuri kiutendaji.

Mwenyekiti wa Michezo Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Wakili Christian Kapere amesema kuwa mpaka sasa maandalizi yanakwenda vizuri wachezaji wote wapo imara kiafya,kiweledi huku akiwa na matarajio lukuki ya kurudi na ushindi kwenye michezo Saba (7) ambayo ORMV watashiriki.

Aidha,ameitaji michezo watakayoshiriki kuwa ni Mpira wa miguu,Mpira wa Pete,kuvuta kamba, Karata, Baiskeli,bao na riadha.

Kapere amemshukuru Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Maendeleo ya Vijana Bi.Jenifa Christian Omolo kwa kuridhia ushiriki wa SHIMIWI,2026 ikiwa ni Mwaka wa awali tangu kuanzishwa kwa Wizara kuwa ametambua michezo ni afya inaondoa magonjwa yasiyoambukiza na kuimarisha utendaji kazi kwa watumishi.