Na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia, Arusha

Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) imefanya semina elekezi kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti leo tarehe 10 Septemba, 2023, mkoani Arusha.

Aidha,semina hiyo ililenga kutoa uelewa kwa kamati hiyo kuhusu majukumu yanayotekelezwa na OSHA na namna taasisi hiyo iliyopo chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu inavyosimamia masuala ya Usalama na Afya katika sehemu za kazi.

Akizungumza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Prof.Joyce Ndalichako wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, amesema masuala ya usalama na afya ni mtambuka na yanagusa sekta zote za uchumi, hivyo ni vyema kushirikiana kuimarisha mifumo ya usimamizi wa usalama na afya kwa wafanyakazi nchini.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Sillo Baran (MB), ameishukuru OSHA kwa mafunzo hayo ambayo yamewajengea uelewa mzuri kuhusu masuala ya usalama na afya. Pia ameitaka OSHA kuendelea kutoa elimu hiyo kwa wafanyakazi nchini ili kuleta tija katika maeneo ya kazi.

Akizungumza awali, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja ameishukuru kamati hiyo kwa kuishauri vyema serikali kuhusu masuala ya usimamizi wa usalama na afya mahali pa kazi na amewahakikishia ofisi hiyo itaendelea kusimamia kwa ufanisi masuala hayo.

Naye, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda amesema taasisi hiyo itahakikisha ustawi wafanyakazi unaimarika sambamba na kulinda uwekezaji kupitia mifumo ya usalama na afya

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati akifungua rasmi mafunzo kuhusu masuala ya Usalama na Afya iliyofanyika katika ukumbi uliopo Gran Melia, tarehe 10 Septemba, 2023, mkoani Arusha.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda akifafanua jambo kuhusu masuala ya usalama na afya wakati wa semina hiyo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Sillo Baran (katikati), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (wa tatu kutoka kushoto), Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Patrobas Katambi (wa pili kutoka kushoto), Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhandisi Cyprian Luhemeja (kulia) na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA), Khadija Mwenda (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati semina ya mafunzo kuhusu masuala ya Usalama na Afya iliyofanyika katika ukumbi uliopo Gran Melia, tarehe 10 Septemba, 2023, mkoani Arusha.
Daktari bingwa wa upasuaji wa Magojwa ya mfumo wa fahamu, Profesa Joseph Kahamba akitoa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti wakati semina ya mafunzo kuhusu masuala ya Usalama na Afya iliyofanyika katika ukumbi uliopo Gran Melia, tarehe 10 Septemba, 2023, mkoani Arusha.
…………
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti, Mhe. Sillo Baran (MB), akieleza jambo wakati wa mafunzo kuhusu masuala ya Usalama na Afya, iliyofanyika katika ukumbi uliopo Gran Melia, tarehe 10 Septemba, 2023, mkoani Arusha.

By Jamhuri