Latest Posts
Tanzania yaonywa kuhusu Al-Shabaab
POLISI wa Uganda wameitaka Tanzania kuwa makini na kundi la ugaidi la Al-Shabaab kutoka Somalia, baada ya jeshi hilo kuwakamata watu wanaotuhumiwa kufanya vitendo vya kigaidi.
Tukio hilo limekuja siku chache baada ya Kenya kujihami kwa Polisi wao kumuua kwa risasi mtuhumiwa wa ugaidi katika maeneo ya Bondeni mjini Mombasa.
Ni Polisi tena
Siku chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kukutana na wadau wa habari na kuwataka waripoti habari zinazozingatia amani na usalama wa nchi pamoja na kuwafanya raia wawe na imani na jeshi hilo, baadhi ya polisi wamekuwa vinara wa kuendeleza vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa raia, huku mara kwa mara wakitumia nguvu kubwa katika utekelezaji wa majukumu yao ya kila siku.
Tanzania yaongoza kuvutia uwekezaji
Imeelezwa kuwa Tanzania imeshika nafasi ya kwanza katika nchi zinazovutia uwekezaji katika nchi za Afrika Mashariki. Kadhalika Tanzania inashika nafasi ya tisa barani Afrika.
Unyonge wa Mwafrika – 1
Naikumbuka vyema Jumamosi ya Mei 30,1969 nilipohudhuria Sherehe za Vijana wa Tanzania zilizofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Upanga, Dar es Salaam na kuhutubiwa na Rais wa Kwanza wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ngeleja; Kichwa kilichojificha nyuma ya tambo za Kikwete
“Natamani kuwa Rais wa mwisho wa Tanzania kuongoza nchi ambayo ni maskini…Nimeongoza nchi maskini, lakini nataka mrithi wangu kuongoza nchi yenye ustawi na utajiri” yalikuwa ni maneno ya Rais Jakaya Kikwete aliyoyatoa Agosti 5, 2014 alipozungumza kwenye Kituo cha Kimataifa cha Maendeleo mjini Washington, D.C., Marekani.
Yah: Ugwadu na utamu wa tunda aujuae mlaji?
Nimesikiliza hotuba nyingi na za viongozi wengi walionona sura zao kwa maisha ya hali bora, wakijaribu kutuzungumzia walaji wa matunda ya umaskini na jinsi tunavyoteseka. Wote nawakubali lakini ni vema nikatoa tahadhari kuwa hayo maisha magumu wanayotuzungumzia wamehadithiwa hawayajui kabisa.