JAMHURI MEDIA

Tunaanzia wanapoishia wengine

Latest Posts

Mwekezaji ahusishwa kifo Katibu wa Chadema

Watu watatu akiwamo Polisi Jamii wa Kijiji cha Ming’enyi, Kata ya Gehandu, Hanang mkoani Manyara, wanadaiwa kumuua Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tawi la Kijiji, Andu Kero.

Lissu amuonya Chenge

*Asema mchezo wa kutumia mahakama haumsaidii

*Amdonoa Rais JK, awatahadarisha wasaidizi wake

*Ataka Jaji Werema afikishwe mahakamani haraka

*CCM yawatosa rasmi Chenge, Prof. Tibaijuka, Ngeleja

 

 

Mwanasheria Mkuu wa chama kikuu cha upinza – Chama cha Maendeleo na Demokrasi (CHADEMA), Tundu Lissu amesema Mwanasheria Mkuu wa zamani wa Serikali, Andrew Chenge anachokifanya mbele ya macho ya Watanzania kwa sasa ni kukwepa kujieleza hadharani.

Ngono: Diwani CCM matatani kugeuza mwanafunzi kimada

Diwani wa Kata ya Nyugwa kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Donald Kabosolo, anafanya kazi ya ziada kuzima tuhuma dhidi yake juu ya uhusiano wa kingono na mwanafunzi wa sekondari ya kata hiyo iliyopo katika  Wilaya ya Nyang’hwale, mkoani Geita.

Kova anawaogopa bodaboda, ataweza uchaguzi?

Wiki iliyopita nimezungumzia hali ya kisiasa katika Jimbo la Lindi Mjini. Nimeeleza katika usuli kuwa hilo la Mama Salma Kikwete kudaiwa kulitaka jimbo hilo ni moja kati ya mambo niliyokutana nayo katika safari ndefu ya kilomita 4,500 niliyozunguka nchi nzima.

Tumerudi mtandaoni, samahani kwa kupotea mwezi mzima

Wapendwa wasomaji wetu salaam, Kwa muda wa mwezi mmoja sasa tangu Januari 29, 2015 mtandao wetu haukuwa hewani kutokana na ujambazi wa mtandaoni (hacking). Hatujui ni nani, ila mtandao wetu ulitekwa na ikawa hatuwezi kuingia kuweka habari au vinginevyo. Kwa…

Salamu za kiuchumi mwaka 2015

 

 

Ndugu wasomaji wa safu hii na gazeti hili, nawasalimu kwa salamu za upendo. Hongera kwa kuwezeshwa na Mungu kuuona mwaka huu mpya wa 2015. Pasipo kujali hali zenu katika maeneo yote; ninaamini lipo tumaini kwa mwaka huu.