Marekani imeionya Palestina dhidi ya maamuzi yake kutotaka kukutana na makamu wa rais Marekani ,Mike Pence katika kikao ambacho kilipangwa kufanyika mapema mwezi huu ili kujadili uamuzi wa rais Trump wa kuhamishia Yerusaleam kuwa mji mkuu wa Israel.

Ikulu ya Marekani imesema, uamuzi huo uliofikiwa na Palestina utakuwa hauna maana kwa kuwa hawataweza kupata suhulu ya mgogoro huo.

Makamu wa rais wa Marekani ana mpango wa kwenda katika ukanda huo wa mashariki ya kati lakini kiongozi wa ngazi za juu wa Palestina ,Jibril Rjoub amesema kuwa kiongozi huyo hakaribishwi Palestina.

Hatua hiyo imekuja mapema baada ya rais Trump kutangaza kuwa anautambua mji wa Yerusaleum kuwa mji mkuu,

Ambapo mpaka sasa Wapalestina takriban 31 wamejeruhiwa katika makabiliano yaliyozuka Ukanda wa Gaza na maeneo ya Ukingo wa Magharibi yanayotawaliwa na Israel kuhusu mji wa Jerusalem.

Please follow and like us:
Pin Share