Polisi wakamata samaki waliovuliwa kwa baruti Dar

Jeshi la Polisi Kikosi cha Wanamaji mkoa wa Dar es Salaam linawashikilia watuhumiwa wawili kwa tuhuma za kukutwa na samaki KG 980 ambazo zilivuliwa ndani ya ndani ya boti yenye usajili wa namba Z.103585 jina MV MAEDRA.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 24, 2023 kwa vyombo vya habari na Kamanda wa Kikosi cha Polisi Wanamaji Dar es Salaam ACP Moshi Sokoro imesema kuwa katika operesheni ya kuzuia uvuvi haramu iliyofanywa na jeshi hilo kwa kushirikiana na Wizara ya Uvuvi na Mifugo Januari 12, mwaka huu, majira ya asubuhi huko maeneo ya soko la Samaki Ferry iliwakamata watuhumiwa hao.

wakiwa katika operesheni ya pamoja ya kuzuia uvuvi haramu na makosa mengine ya kijinai walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao.

Jeshi la Polisi limewapongeza wananchi wote ambao wanachukia uhalifu na limewaomba waendelea kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili hatua stahiki zichukuliwe kwa wahalifu hao.

Pia Jeshi hilo limetoa onyo kwamba halitasita kuchukua hatua kwa yeyote atakayejihusisha na uvuvi haramu pamoja na makosa mengine ya kijinai.