Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ametengua nafasi mbalimbali za viongozi wakiwemo nwakurugenzi na wakuu wa wilaya.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 24,2023 Ikulu na kusainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikuku, Zuhura Yunus, Rais ametengua uteuzi wa Reuben Ndiza Mfune, Mkuu wa Wilaya ya Mbarali.

Pia ametengua nafasi za Wakurugenzi Watendaji ambao ni Msongela Nitu Palela, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Mara;Michael Augustino Matomora, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Singida.

Pia ametengua uteuzi wa Linno Pius Mwageni, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu, Shinyanga; na Sunday Deogratius Ndori, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa, Njombe.

Utenguzi huu ulianza tarehe 22 Januari,2023.

By Jamhuri