Na Abel Paul,Jeshi la Polisi, Dodoma

Jeshi la Polisi nchini limetoa ufafanuzi wa taarifa iliyo ripotiwa katika baadhi ya vyombo vya Habari ambayo ilikuwa na kichwa cha habari kisemacho, kashfa Polisi yahusishwa na kutekwa kwa Baba na mwanawe.

Akitoa taarifa hiyo leo msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamshna msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP David Misime amesema kuwa taarifa hiyo ilieleza kuwa waliopotea ni Damas Bulimbe na mwanae Lucas Bulimbe huku taarifa hiyo ikieleza kuwa walipotea toka tarehe 15.11.2023

SACP Misime amesema kuwa baada ya Baba huyo kumdhamini mtoto wake kutoka katika Kituo cha Polisi Kakubilo kilichopo Busanda Mkoa wa Geita alikokuwa anashikiliwa kwa tuhuma za mauaji ya shangazi yake aitwaye Nyamiti Bulimbe Novemba 8, 2023.

SACP Misime ameeleza kuwa kwa mujibu wa uchunguzi uiofanywa na Jeshi hilo hadi sasa familia hiyo ipo kwenye uhasama mkubwa kutokana na mgogoro wa kugombea shamba lililoachwa na Bulimbe Mswaga aliyefariki dunia.

Ameongeza kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wa tukio hilo ambapo linashirikisha maafisa wengine wa Jeshi hilo kutoka makao Makuu ya Jeshi la Polisi ili kubaini na kupata ushahidi wa watu waliohusika katika Mauaji ya Nyamiti Bulimbe.

Pia Msemaji wa Jeshi hilo amesema Jeshi la Polisi litaendelea kuchunguza kwa karibu taarifa zote za watu ambao zimetolewa kutokana na kupotea ili ukweli utakapopatikana.