Na Mussa Augustine,JamhuriMedia

Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof Adlof Mkenda a amelitaka Baraza la taasisi ya Elimu ya watu wazima(TEWW) kuhakikisha utoaji wa elimu bila ukomo unakua endelevu

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es salaam katika ziara yake alipotembelea Taasisi ya Elimu ya watu wazima ambapo amesema serikali imeendelea kufanya mapitio ya mitaala ya kuwa inaakisi mfumo mpya wa utoaji wa elimu yake na kukusanya maoni kutoka kwa wadau mbalimbali.

“Haya mambo mawili sera mitaala na linafanyikaga kwa wazi lakini sula la miundo hufanyika kimyakimya kwani kwani mara zote kuna kuwaga na shinikizo kuwa mitaala ipitiwe kuhakikisha linaendana na ufanisi wa elimu tofauti muundo ” amesema Profesa Mkenda

Hata hivyo amesema pia sera ipo ya elimu bila ukomo lakini hutegemea taasisi nyingi ikiwemo za binafsi na serikali hivyo taasisi ya elimu ya watu wazima haina budi kujitathimini ni kwa namna gani elimu bila ukomo inatolewa bila kuangilia umri .

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Sayansi Elimu na Teknolojia Prof Carolyne Nombo amesema siyo watu wote wanajua kisoma na kuandika hivyo taasisi hiyo ihakikishe inakuwa na vituo kila mahali hadi vijivini kusaidia wale ambao wana umri mkubwa waliashindwa kwenda shule kutokana na changamoto mbalimbali ili wajiunge wafundishwe kwani hawawezi kuchanganywa na watoto wadogo

Naye Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima Pfofesa Michael Ngumbi amesema TEWW ina jumla ya vituo 605 mwaka wa masomo 2022/2023 hivyo kwa ujumla katika kipindi cha miaka hiyo miwili kulikuwa na wanufaika wapatao 6238 ambapo imeendelea kutoa mafunzo kwa waalimu na wasimamizi wa elimu ya watu wazima kupitia programu za kawaida na elimu masafa katika kampasi za Dar es salaam , Mwanza, Morogoro, .

Sambamba na hayo amesema taasisi hiyo wameshatengeneza mtaala wa kutoa mafunzo wa stashahada na ikishapitishwa na baraza la mitihani NACTE mwaka huu tunaweza tukaanza kutoa mafunzo Mungu akijalia

“Kwetu sisi tayari kupitia elimu ya watu wazima mafunzo mengi yanajikita katika ujuzi kupitia programu za IPOSA na IPPE na kwa sasa tunaandaa programu mpya ambayo ambayo itawaandaa waalimu wa elimu ya watu wazima waliobebea katika kufundisha maeneo mbalimbali ya ufundi wa kihandisi,na ufundi na programu hiyo mpya inaitwa stashahada ambapo maandalizi yake yapo katika hatua ya kuwashirikisha wadau watoe maoni yao”amesema Profesa Michael

Sanjari na hayo amesema katika kipindi cha miaka mitatu 2020/2023 TEWW ilipatiwa jumla ya TZS bilioni 9.4 ili kusaidia kutekeleza shughuli za mradi wa SEQUIP hivyo fedha hizo zimetumika katika kuboresha ikiwemo ujenzi wa ofisi, madarasa , pia ilitoa serikali TZS milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo jengo la utawala katika Kampasi ya Morogoro na liko katika hatua ya mwisho .

“Tunatarajia kuzindua kampasi kampasi mpya mbili za Ruvuma na Kilimanjaro katika mwaka wa masomo 2023/2024 na kuimarisha shughuli za uratubu vituo mikoani kwa kuongeza watumishi” amesema Prof Michael

Aidha taasisi ya TEWW inatekeleza majukumu yake kwa mujibu wa Sheria ya Elimu ya watu wazima na 12 ya mwaka 1975 na inaongozwa na mkakati wa kitaifa wa kisomo na Elimu ya Umma

By Jamhuri