Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dkt.Hussein Ali Mwinyi ametembelea Bandari ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika ziara ya kushtukiza na kushuhudia karafuu za magendo tani 9.5 zenye thamani ya shilingi milioni 140 zilizotaka kusafirishwa kwa magendo na kukamatwa kwa ushirikiano wa Vyombo vya ulinzi na usalama Mkoa wa Kaskazini Pemba vikiwemo Mamlaka ya Kuzuia Rushwa na Uhujumu Uchumi Zanzibar (ZAECA) na Kikosi cha Kuzuia Magendo (KMKM) tarehe 04 Januari 2024 , Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Aidha Rais Dkt.Mwinyi ameleeza kuwa Serikali imeamua asilimia 80 ya mauzo ya karafuu katika soko la dunia kumpatia mkulima wa karafuu na 20 kwa shirika la biashara Zanzibar (ZSTC) kutumika katika uendeshaji.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi amesema karafuu iliyokuwa bora inatoka Zanzibar kwa kuitunza vizuri na kuisafisha bei yake itaendelea kuimarika duniani.

Halikadhalika Rais Dkt.Mwinyi amewasihi wananchi wasifanye magendo kwa maana watapata hasara kulingana na sheria za nchi, pia amesema Serikali itaendelea kuongeza bei ya karafuu.