Rais Mwinyi azindua muongozo wa mafunzo ya sayansi,kiingereza na hisabati

Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kulia) akisalimiana na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Lela Mohamed Mussa na Naibu wake Mhe.Ali Gulam Hussein pamoja na Viongozi wengine mara alipowasili katika hafla ya  Uzinduzi wa muongozo wa mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari  katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar,mafunzo hayo yataendeshwa na Shirika  la Koika
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia) akimsikiliza Meneja mwandamizi wa Goodneighbors  Nd.John Massenza akitoa maelezo wakati alipotembelea maonesho ya Vitabu mbali mbali vya kufundishia  katika hafla ya  Uzinduzi wa muongozo wa mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari  nje Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar,ambapo Shirika  la Koika litaendesha mafunzo hayo.
Viongozi mbalimbali wakiwa katika hafla ya Uzinduzi wa muongozo wa mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari yatakayoendesha na Shirika la Koika hafla iliyofanyika leo katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar,mgeni rasmi akiwa Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (hayupo pichani).
Rais  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi (kushoto) akizungumza wakati wa  Uzinduzi wa muongozo wa mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari yatakayoendesha na Shirika la Koika katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege Zanzibar (kulia) Balozi wa Korea Kusini Nchini Tanzania Mhe.Sun Fyo Kim na Mkurugenzi Mkaazi  wa KoikaTanzania Bw.Kyucheol Eo.
Baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi.(hayupo pichani) akihutubia na kuzindua Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi kwa Skuli za Sekondari Zanzibar, uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip Uwanja wa Ndege Kiembesamaki Wilaya ya Magharibi “B” Unguja leo 3-8-2022
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa Vitabu vya Muongozo wa Mafunzo ya Sayansi,  Hesabati na Kingereza na Balozi wa Korea ya Kusini Nchini Tanzania Mhe. Sun Pyo Kim (kulia kwa Rais) na Mkurugenzi Mkaazi wa KOICA Tanzania Bw.Kyucheol Eo na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhandisi Zena Ahmed Said na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Lela Mohammed Mussa, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja Mhe.Idrisa Mustafa Kitwana  na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe. Ali Abdulgulam Hussein.(Picha na Ikulu)