na Mwandishi Wetu, JamhuriMedia,

Ikiwa ni siku moja tangu Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Paul Makonda kupokea changamoto ya kijana Alhaji Yahya Abdallah ambaye anafanya biashara ya kuuza ndizi ili kumsaidia mama yake na wadogo zake wanne na Mwenezi Makonda kwa niaba ya CCM kumuahidi kumsomesha na lumpatia kiasi cha fedha kwa ajili ya vitendea kazi na sare za shuleni.

Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha kuguswa zaidi na jambo hilo na kumsaidia mwanamama huyo mjane kwa kumpatia kiwanja na kumjenga nyumba kubwa ya kuishi na watoto wake wote ambapo ujenzi wa nyumba hiyo utaanza Ijumaa Februari 9, 2024.

Pia, Dkt. Samia ameahidi kuwasomesha watoto wote watano wa mwanamama huyo pamoja na kugharamiwa vifaa vyote vya shule na sare.

Aidha, Dkt. Samia amempatia mwamamke huyo kiasi cha Tsh milioni 5 itakayokuwa inatolewa kupitia Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Kigoma Mjini kwaajili ya kufanya shughuli zake za biashara kujikwamua kiuchumi.

Vilevile, Dkt. Samia kumgharamia mwanamama huyo huduma ya afya kwa kumagizia Mkuu wa Mkoa wa Kigoma kuhakikisha mwanamama huyo mjane anafikishwa hospitali na kufanyiwa uchunguzi wa tatizo alililonalo la uvimbe tumboni na kupatiwa matibabu.

Hayo yote yamewasilishwa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo Ndugu. Paul Makonda, mnamo Februari 04, alipofika nyumbani kwa Mwanamama huyo mjane kumtembelea na kutoa salamu hizo za upendo kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

By Jamhuri