Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewateua wafuatao

Amemteua Tito Philemon Mganwa kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Korogwe; na (ii) Amemteua Bw. Mussa R. Kilakala kuwa Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora.

Aidha, Rais amefanya mabadiliko madogo ya vituo vya kazi kama ifuatavyo:

Athumani Francis Msabila kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujji kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya lgunga; Mwantum Hamis Mgonja kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Igunga kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji; na

Mwamvua Bakari Mnyongo kutoka Wilaya ya Kaliua Mkoa wa Tabora kwenda kuwa Katibu Tawala Wilaya ya Chemba, Mkoa wa Dodoma. Zuhura Yunus Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais,