Rais Samia akiwa kwenye ashiriki Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru Manyara

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwapungia mkono Vijana wa hamasa wakati alipokuwa akielekea kukagua mabanda ya Maonesho ya Vijana Kitaifa Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Wakuu wa Mikoa pamoja na viongozi wengine wakiwa kwenye Sherehe za mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Matembezi ya Vijana yakipita mbele ya Jukwaa Kuu wakati wa Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akipokea Ripoti ya Mbio za Mwenge Kitaifa 2023 kutoka kwa Kiongozi wa Mbio hizo Abdallah Shaibu Kaimu wakati wa Maadhimisho hayo katika uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Shamrashamra za Maadhimisho ya Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo Kitaifa zimefanyika Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Wageni mbalimbali waliohudhuria maadhimisho za mbio za Mwenge wa Uhuru ambazo Kitaifa zimefanyika Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akitoa vyeti kwa wakimbiza Mwenge Kitaifa katika Kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru ambayo Kitaifa yamefanyika kwenye uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati Mkoani Manyara tarehe 14 Oktoba, 2023.