Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimfariji muathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Bi. Salome Elifuraha ambaye amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini iliyopo Katesh, Hanang. Mama amepoteza watoto wawili kwenye maafa hayo huku mtoto wa tatu akiwa bado hajapatikana hadi sasa. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika hospitali hiyo ya Wilaya Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa eneo la Jorodom ambalo limeathirika na Mafuriko pamoja na maporomoko ya matope na mawe Wilayani Hanang mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Rais Samia alijionea uharibifu mkubwa uliotokea na kuwapa pole Waathirika wa maafa hayo na kuwaeleza kuwa Serikali ipo pamoja nao.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Ndugu Elibariki Naman mkazi wa Jorodom, Katesh ambaye ni muathirika wa Mafuriko yaliyotokea Wilayani Hanang. Ndugu Elibariki alikuwa akielezea jinsi majirani zake walivyopoteza maisha pamoja na makazi yao katika maafa hayo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Manyara Mhe. Queen Sendiga akielezea kuhusiana na athari za mafuriko yaliyotokea katika eneo la Jorodom Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia ametembelea eneo hilo Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.

By Jamhuri