Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta na Mkuu wa Mkoa wa Manyara Queen Sendiga wakati wakiangalia athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ndani ya Helikopta wakati akiangalia athari za mafuriko yaliyotokea katika mji mdogo wa Katesh pamoja na vijiji jirani, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akimjulia hali Bi. Christina Nyangole pamoja na mtoto wake Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang Mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023. Bi. Christina na mtoto wake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh, Hanang mkoani Manyara.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa amembeba mtoto Wina Joseph mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi 8 ambaye pia yeye na mama yake ni waathirika wa mafuriko yaliyotokea Katesh Wilayani Hanang. Rais Samia aliwatembelea majeruhi wa maafa ya mafuriko hayo ambao wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tumaini, Hanang mkoani Manyara tarehe 7 Desemba, 2023.
ais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Waathirika wa Mafuriko waliopo kwenye kambi zao Katesh, Wilayani Hanang mkoani Manyar

By Jamhuri